SOMA TAARIFA MPYA KUHUSU MTOTO KUJIPIGA RISASI!🔻

0

 

Mtoto mwenye umri wa miaka 6, Erick Mkandi ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Izumangambo Mkoani Geita, amefariki dunia wakati akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Bwanga baada ya kujipiga risasi kwenye paji la uso na ikatokea kisogoni akiwa ndani ya chumba cha Baba yake.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limesema tukio hilo limetokea November 13, 2021 katika Kitongoji cha Mkapa Kijiji cha Izumangambo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema silaha aliyoitumia Mtoto huyo kujipiga risasi ni aina ya pistol Berreta yenye namba TZS AR74955/E.86808Y ambayo inamilikiwa kihalali na Baba yake Mzazi aitwaye Joshua Faustine  huku chanzo cha tukio kikiwa ni mtoto kutokujua madhara yatokanayo na utunzaji mbaya wa silaha hiyo.


"Niwaombe Wamilki wote wa silaha wawe makini katika kutunza silaha zao kwani wanapokuwa wanakabidhiwa wanaelekezwa namna ya kutunza silaha hizo" — Kamanda Mwaibambe.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top