KIFUNGU CHA 113 CHA KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 ILIYOREJEWA MWAKA 2019 KINASEMA;
Mtu yeyote ambaye-
(a) anatangaza kutoa zawadi kwa kurejesha mali yoyote ambayo imeibiwa au imepotea, na katika kutoa zawadi hiyo ametumia maneno ikionyesha kwamba hakuna maswali yatakayoulizwa, au huyo mtu anayetoa mali hiyo hatakamatwa au kudhuriwa; au
(b) anatangaza hadharani kumrejeshea mtu yeyote ambaye atanunua au ametanguliza malipo ya fedha kwa njia ya kukopa kwa ajili ya mali yoyote iliyoibwa au kupotea, mali hiyo iliyolipwa au kutanguliwa au kiasi kingine chochote cha fedha au zawadi kwa ajili ya kurejeshwa kwa mali, au
(c) anachapisha au anatangaza ahadi kama hiyo, kama ilivyotajwa katika aya ya (a) au (b), atakuwa ametenda kosa.
Imeandikwa na Mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_)
Wa Jungu la sheria Tanzania
0758218269/0628729934