WANANDOA WATUHUMIWA KUMUUA BOSI WAO KAGERA

0


Wanandoa wawili waliokuwa wakifanya kazi za vibarua, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kumuua mwajiri wao Theopista Laurent (71) mkazi wa Kijiji cha Buharata wilayani Missenyi wakidai kuwa kawatumikisha muda mrefu bila kuwalipa ujira wao.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Awadhi Juma, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa bibi huyo aliuawa Oktoba 15, 2021, na kwamba baada ya watuhumiwa hao ambao ni Robert Berenado (19) na mke wake Benadetha Robert (19) kutekeleza mauaji hayo walikimbia na kwenda kujificha katika Kijiji cha Kiruruma kilichoko wilayani Karagwe, na baada ya upelelezi kufanyika walikamatwa na Polisi Oktoba 31, mwaka huu.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top