Ameendelea kusema kuwa mfuko huo utatoa shilingi 500,000 pindi mtumishi atakapofariki au kufiwa na ndugu wa karibu wakiwemo baba, mama, mke,mume pamoja na Watoto wanne ambao mtumishi atakuwa amewaandikisha kwenye orodha ya wategemezi itakayoandaliwa na kwamba fedha zitakazokusanywa zitawekwa kwenye akaunti maalumu na kusimamiwa na kamati maalumu ya watu wasiozidi watano.
Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Tamko Mohamedi amesema kuwa uwepo wa mfuko huo haiondoi stahiki kama hizo anazostahili kuzipata mtumishi kutoka kwa mwajiri na kusisitiza kuwa mfuko huo ni wa hiyari hivyo wanufaika ni watumishi ambao wataridhia kukatwa kwenye mshahara kwa kujaza fomu maalumu.
Aidha amewataka Wajumbe wa Baraza hilo kila kmmoja kwa uwakilishi wake akafikishe hoja hiyo kwa watumishi anaowawakilisha ili kila mtumishi aweze kuridhia kujiunga na mfuko huu muhimu wa kufa na kuzikana