WAZIRI MAJALIWA ATOA AGIZO JIPYA KAMATI ZA UJENZI WA MIRADI KOTE NCHINI.

0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo wilaya ya Ruangwa, hivyo ni lazima fedha hizo zitumike kama ilivyokusudiwa.

 

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameagiza kwamba wenyeviti wote wa kamati za ujenzi wa mradi hiyo ikiwemo ya ujenzi wa vituo vya afya pamoja na shule watoke katika vijiji ambavyo miradi husika inatekelezwa ili kurahisisha usimamizi.

 

Ameyasema hayo Novemba 22, 2021) wakati akikagua ujenzi wa shule ya Sekondari Kitandi iliyoko Kata ya Likunja wilayani Ruangwa, Lindi akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Lindi.

 

Waziri Mkuu amewataka watu wote walioko kwenye kamati zinaosimamia miradi hiyo  wawe waadilifu na wahakikishe wanadhibiti vitendo vya wizi katika maeneo yote yanayotekelezwa miradi na ijengwe kwa viwango. 

Lazima tuzilinde fedha zilizotolewa na Rais wetu mpendwa.”

 

Amesema kuwa mpango wa Mheshimiwa Rais  Samia ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma zote za kijamii ikiwemo Afya, maji, umeme, barabara ili kuwarahisishia kutekeleza shughuli zao 

“maendeleo haya yote ni kutokana na juhudi za mkuu wa nchi, lazima tumuunge mkono”

 

Kiongozi wa nchi ametoa fedha, hatuwezi kuvumilia kuona mtu mzembe kwenye miradi ya Serikali, huu ni ujumbe kwa kamati zote zinazosimamia ujenzi wa miradi nchini. Wananchi wanatajaria kuona miradi hii inakamilika, simamieni miradi na iishe tena kwa viwango, Mheshimiwa Rais Samia anatoa fedha kwa ajili ya miradi hii ya wananchi”

 

Waziri Mkuu amesema kuwa wajumbe wote wa kamati za ujenzi wa miradi nchini washirikishwe kwenye hatua zote za ujenzi ikiwemo ununuzi wa vifaa vya ujenzi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top