CCM NJOMBE WAPINGANA NA MAAGIZO YA SERIKALI WALIOPATA MIMBA KUREJEA SHULENI.

0

 Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu serikali kutangaza kuwa sasa ni ruksa kwa wanafunzi waliokatishwa masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo waliopata mimba,chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Njombe kimeonesha kutokukubaliana na maamuzi hayo na kushauri serikali ibadili maamuzi yake.

Akitoa Maazimio ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Njombe, Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya Njombe, Hitla Msola amesema hawajaridhishwa na maamuzi ya serikali ya kuruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kurejea shuleni.

"Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Njombe haijalikubali hilo jambo na imependekeza jambo hilo kusitishwa kitaifa kwa sababu sio jambo zuri inakiuka tamaduni na mila zetu,hili jambo halikubaliki la watoto waliopata mimba kutakiwa kurejea shuleni"amesema Msola.

Msola amesema huwezi kukawa na wanafunzi waliokwisha kupata mimba na wengine hawajapata akidai kuwa utakuwa unafundisha kitu gani kwati ya makundi hayo mawili.

alipohojiwa zaidi na waandishi wa habari juu ya kupingana na serikali amesema wao kama halmashauri kuu ya wilaya wanaomba yafanyike mabadiliko.

Aidha Azimio lingine kati ya manne yaliyotolewa kwa waandishi na Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya Njombe, Hitla Msola amesema kupitia halmashauri hiyo hawakubaliana na kuzuiwa kwa tuition kwa shule na kuishauri serikali kurudisha tuition ili kuepuka kutumia muda mwingi kutazama TV.

'Hilo haliwezi kutuzuia sisi kutafuta wale walimu wa kawaida ,miminiwaasa kama mwenezi bado kuna walimu wa shule za private (Binafsi) wanatoa tuition unaweza kutumia mbinu mbadala wakati unasubili tamko tena la serikali ila tuendelee kutumia hizo tuition kwa ajili ya watoto wetu ili kupata maendeleo ya kitaalum" amesisitiza Msola.

Mazimio mengine yalitolewa ni pamoja na kumpongeza Rais samia kwa kazi ya kuliongoza taifa,pamoja kuongeza bajeti kwenye TARURA ili kuongeza uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa kuwa mkoa wa Njombe una fursa nyingi za kiuchumi.

Itakumbukwa kuwa kwa sasa Utekelezaji wa Maagizo ya serikali ya Kuruhusu wanafunzi waliokatishwa masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba limeanza kutekelezwa ikiwa sambamba na kuzuia masomo ya ziara kwa wanafunzi hasa wakati huu wa Likizo ya mwisho wa mwaka na mwaka mpya ili wanafunzi wapate kufanya mambo mengine.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top