KABLA YA KUFUNGA NDOA UNATAKIWA KUZINGATIA SHERIA HII KABLA

0

  SHERIA YA NDOA, ya mwaka 1971 Sura ya 29 ya mwaka 2002 kuanzia kifungu Cha 18 na kuendelea, inaelezwa kabla ya kufunga NDOA ni HATUA gani zitazingatiwa Kama ifuatavyo;

Kifungu Cha 18, wanandoa watarajiwa wanatakiwa kutoa taarifa/notisi kwa maandishi kwa msajili wa NDOA siku 21 kabla ya tukio la NDOA yenyewe. Na msajili hapa anayetakiwa kupewa taarifa anaweza kuwa Padre, sheikh, mchungaji n.k na ni lazima msajili huyo awe amesajiliwa na kupewa leseni ya kufungisha NDOA.


Notisi au taarifa kwa msajili wa NDOA inatakiwa ionyeshe yafuatayo;

1. Majina ya wanandoa watarajiwa, umri wao na mahali wanapoishi.

2. Majina ya wazazi wao na mahali wanapoishi wazazi wa pande zote mbili.

3. Maelezo yanayoashiria kuwa mahusiano yao ni Halali na hayajazuiwa kisheria.

4. Maelezo kwamba NDOA inatarajiwa kuwa ya mke mmoja au wengi.

5. Maelezo ya pande zote mbili juu ya Hali zao za kimahusiano kabla ya kufunga ndoa, Kama ni mjane, mgane n.k

Na mengineyo mengi kulingana na Hali au mazingira ya ndoa yenyewe.


Kifungu Cha 19, baada ya msajili kupata taarifa/notisi ya nia ya NDOA, atatakiwa kuiweka hadharani ijulikane kwa umma, na mtu yeyote mwenye pingamizi ataruhusiwa kuweka pingamizi lake Kama kifungu Cha 20 kinavyoonyesha.


Kifungu Cha 22, Endapo Kama kutakuwa na pingamizi, yatafanyika mapitio kwenye pingamizi kubaini Kama kuna sababu za msingi za kusitisha ndoa hiyo mpya kufungwa au kuendelea kufungwa kwa ndoa hiyo.


Kama hakutakuwa na sababu za msingi, ndoa hiyo itafungwa, kutofungwa kwake kutatokana na sababu za msingi za muweka pingamizi mfano; 

1. Kama mwanandoa mtarajiwa tayari ana NDOA nyingine Halali na ndoa hiyo ilikuwa ni ya mke mmoja.

2. Endapo ndoa ni ya wake wengi na MKE anataarifa za kuthibitika kuwa MKE mwenza mtarajiwa anatabia chafu au ugonjwa mkubwa wa zinaa n.k hasa katika ndoa za kiislamu.


Imeandikwa na mwanasheria

Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_ )

Wa Jungu la sheria Tanzania.

0758218269/0628729934.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top