MH.Ummy Sijaridhishwa na Ujenzi wa Kituo cha Afya Kisisiri, Iramba.

0

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo cha Afya Kisisiri kinachoendelea kujengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

Waziri ummy ameyasema hayo wakati wa ziara yake Wilayani humo na kutembelea kitua hicho kukagua maendeleo ya ujenzi na kukuta ujenzi ukiwa kwenye hatua ya kupandisha kuta ilihali maeneo mengine wako kwenye hatua za umaliziaji.


‘ sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hiki bado mko nyuma sana na kwa hapa mlipofikia hatuwezi hata kuwaletea fedha za awamu ya pili kwa sababu haya majengo ya awamu ya kwanza hayaridhishi yalipofikia’ alisema Mhe. Ummy


Nimepita maeneo mengi nimekagua vituo vya Afya vilivyopata fedha sawa na hiki chenu cha Kisisiri lakini vingi wameshaezeka wako kwenye hatua za umaliziaji lakini nyie hapa ndio kwanza mnapandisha kuta kwa kweli sijaridhishwa kabisa na hatua hii’


Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Sophia Kizigo amesema watahakikisha wanaongeza usimamizi ili ujenzi wa kituo  hicho uendane na muda uliopangwa.


Kituo cha Afya Kisisiri Wilayani Iramba kilipata fedha za tozo za miamala ya simu tsh milioni 250 kwa ajili ya kujenga majengo ya awali yanayotakiwa kwa ajili ya kufungia Kituo cha Afya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top