MKUU WA MKOA WA NJOMBE ALIONYA BARAZA LA MADIWANI WILAYA YA MAKETE KULUMBANA NA MKURUGENZI!

0

Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani la dharura


Mwenyekiti Wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Mh.Francis Chaula akizungumzia maamuzi ya Barua waliyoandika kwenda kwa waziri Wa Tamisemi kuhusu malalamiko yao

Baraza la madiwani la dharura likiendelea ambapo katika kikao hicho hawakuweza kuvaa majoho kama kwenye mabaraza ya kawaida

Na;Edwin Moshi Greenfm

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe wametakiwa kuondoa tofauti zao na kushikamana kuwa kitu kimoja kwa kuwa athari za malumbano wanayoyaendeleza tayari zimeonekana kuathiri shughuli za maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya ameyasema hayo Desemba 21, 2021 katika kikao chake cha dharura na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Makete alichoagiza kiitishwe kutokana na sintofahamu iliyojitokeza ya malalamiko ya kimaandishi yaliyopelekwa kwa Waziri  mwenye dhamana kulalamikia baadhi ya mambo katika halmashauri hiyo kuwa hayaendi sawa.


Miongoni mwa aliyoyasema na Mkuu wa Mkoa ni pamoja na halmashauri ya Wilaya ya Makete licha ya kupewa ujenzi wa vyumba vichache vya madarasa vya mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya COVID - 19 ukilinganisha na halmashauri nyingine za mkoa wa Njombe, lakini mpaka sasa vyumba hivyo havijakamilika hali aliyodai imechangiwa na malumbano baina ya viongozi wa Halmashauri na Barza hilo yasiyo na tija.


'Katika halmashauri zote za mkoa wetu Halmashauri ya wilaya ya Makete ilikuwa na vyumba 24 hivyo vyote vilitengwa kutokana na bajeti tuliokuwa tumewasilisha lakini kwa bahati mbaya wakati halmashauri zingine kwa mkoa wa Njombe zikiwa zimekamilisha zingine zikiwa hatua ya mwisho lakini Halmashauri ya wilaya ya Makete hatujakamilisha hata chumba kimoja mnaendeleza malumbano yenu mimi niseme yanayoendelea kwenye Halmashauri yetu ni aibu' Amesema Rubirya

Katika kikao hicho mkuu wa mkoa amefika na barua iliyodaiwa kuandikwa na madiwani hao kwenda kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ikimtuhumu Mkurugenzi wa Halmashauri kuzuia baraza lisitekeleze majukumu yake kwa kudharau kutengua na kufuta maazimio na yatokanayo katika makabrasha ya mikutano ya baraza la Madiwani kinyume na mabaraza mengine katika mkoa wa Njombe ambapo mkuu huyo wa mkoa kupitia kwa mwanasheria wa kutoka ofisi yake akatoa ruhusa ya kusomwa kanuni ya 13 na 14 za mabaraza ya madiwani kutoka halmashauri nyingine za mkoa wa Njombe ambazo zimeonekana hazina utofauti na za Makete 

Hali hiyo ikamfanya Mkuu wa mkoa kusimamia zoezi la kupiga kura za maandishi za ndiyo au hapana ili kubaini iwapo barua hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ikiwa imendikwa kwa baraka za madiwani hao ama la! ambapo matokeo yameonesha kura za Ndiyo 11 na za Hapana 19, na kwamba kwa matokeo hayo, madiwani 11 wamesema ndiyo wanaitambua na madiwani 19 wakisema Hapana hawaitambui.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema barua hiyo imekwenda mahala ambapo sio sahihi na kusema wanaodhani kwamba mkuu wa Mkoa ni mtu mdogo wanakosea kwani yeye pamoja na mkuu wa wilaya ni watu wakubwa ambao wamepewa dhamana ya kusimamia mambo katika maeneo yao ya kiuongozi

Baadhi ya madiwani akiwemo Simion Mwaikenda, Feliks Kyando, Abel Mahenge na Ernesta Lwilla wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusu barua hiyo ambapo wengine wamesema ni makubaliano ya madiwani huku wengine wakisema si makubaliano ya wote

'Mh.Mkuu wa Mkoa ni kweli Mkurugenzi tulikutana nae tukazungumza nae alifikiaa kipindi kuwa yupo tayari kuinua wilaya ya Makete,sisi madiwani ndio tulioyajadili lakini leo tunayageuka lazimatuzungumze kitu kilichowazi' amesema Felix Kyando.

'Tulipoingia kwenye kikao cha baraza la madiwani siku hiyo tulienda vizuri na kupata mafafanuzi kwa kufuata kanuni na taratibu sasa hiyo tarehe 9/novemba 2021 iliyokuwa inaandikwa barua ndio hawa wanaosema mengine hayamo hayamo ndio waliomwambia mwenyekiti hebu njoo tukae hapa tuandike hiki na hiki ndugu zangu tunakwenda wapi? wananchi wanasubili maendeleo hawasubili malumbano tunayoendeleza hivi sasa' Ernesta Lwilla 

Baada ya majadiliano Mkuu wa Mkoa alitoa nafasi kwa Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Francis Chaula ambaye ndiye aliyeiandika barua hiyo kwenda kwa Waziri kusema neno,ambapo Mh Francis Chaula ameanza kwa kushukuru ujio wa mkuu wa Mkoa na kusema hilo la barua lilifanyika ili kushinikiza utekelezaji wa maagizo yaliyoagizwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe baada ya kuona hayafanyiki


Mwenyekiti huyo amesema binadamu yoyote ana mapungufu hivyo makosa yaliyofanyika kwa kumwandikia barua Waziri ni mapungufu ya kibinadamu hivyo kuomba wao kama madiwani waanze upya na baraza lipewe ushirikiano ili shughuli za maendeleo zisonge mbele


'Mh.Mkuu wa Mkoa ninakushukuru kwa ujio wako na niwaomba waheshimiwa Madiwani tulioandika hii barua imekwenda kule leo mkuu wa mkoa kaja hapa tuyamalize,nimuombe Mkurugenzi afanya kazi na Baraza hili,mimi mhimili wangu ni madiwani wakisema Mwenyekiti hutoshi kwa kweli nitakuwa sitoshi wakisema endelea naendelea sasa nikisema namsikiliza Mkurugenzi madiwani nawapinga mwisho wa siku atakaye niondoa ni madiwani hivyo kwa haya yanayoendelea sisi ni binadamu tunamapungufu Mheshimiwa mkuu wa Mkoa tunaomba utusamehe bure pamoja na madiwani wangu inawezekana kila mmoja alikuwa akitafuta pakutokea'.Amesema Francis Chaula


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Jasel Mwamwala ametoa onyo kwa madiwani hao na kusema ipo kamati ya maadili ya Chama ambayo haitasita kuwaita madiwani wanaoonekana kukwamisha shughuli za maendeleo na wataweza kupoteza udiwani wao

'Lakini ndugu zangu tuone tulivyojianika tuone tulivyokaa mkurugenzi wenu anamiezi miwili leo tunaamua kumkataa hivi tumejifunza tumemjua vizuri huyu mkurugenzi?,sasa sisi chama tukisema tuchukue hatua wengine mtapoteza udiwani wenu hapa' amesema Mwamala. 


Mwamwala pia amemtaka Mwenyekiti wa Halmashauri kuangalia ushauri anaopewa na madiwani wenzake na auchuje kabla ya kufanya maamuzi huku pia akiwaonya madiwani wanaompotosha kuacha kufanya hivyo 

'Mpo mnaaompotosha Mwenyekiti wa Halmashauri,Mwenyekiti wa Halmashauri tumia zako hamsini usitegemee hamsini za wenzako,ukitumia hamsini za hawa wenzako utaharibikiwa chonde chonde zingatieni yaliyowaleta hapa sio malumbano' Amesema Mwamala.


Ndipo Mkuu wa mkoa Mhandisi Marwa Rubirya akawataka madiwani hao kumaliza tofauti zao na wafungue ukurasa mpya kwa kuwa huu sio muda wa kuendeleza malumbano kwa sababu yapo mengi ya kusimamia kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya ya Makete na Mkoa kwa ujumla

'Mimi niombe twendeni tukafungue ukurasa Mpya Makete afu Makete mlikuwa na picha tofauti hata tuliyoyafanya kule Dar es Salaam na MDA si wilaya nyingi zinaweza zikafanya mambo kama yale'amesisitiza Rubirya.

  


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top