Rais wa Tanzania, Samoa Suluhu Hassan ameyaonya makundi yanayochafua Serikali yake ya awamu ya sita kwa kusema kuwa ufisadi umerudi na mambo yako hovyo.
Akizungumza Jumamosi Desemba 4, 2021 wakati akizindua gati katika Bandari ya Dar es Salaam, amesema kuna makundi ndani ya Serikali wanajua wanayoyafanya ingawa yanageuka na kusema Serikali hii ya awamu ya sita ufisadi umerudi.
“Kuna makundi wanayajua wanayoyafanya ndani ya serikali ni makundi hayo hayo yanageuka kusema Serikali ya awamu ya sita ufisaidi umerudi, mambo yako hovyo, kumbe wao ndio wako hovyo.Na mambo yale hayakufanyika ndani ya awamu ya sita, yalifanyika huko nyuma gari bovu linaangushiwa awamu ya sita sitakubali. Niliapa kusimamia haki za wananchi, nitasimama nao”.Rais Samia Suluhu Hassan