KUTOA MIMBA NI KOSA LA JINAI TANZANIA LENYE ADHABU MPAKA YA MIAKA SABA JELA.
KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KIFUNGU CHA 151.
Kifungu hicho kinasema, mwanamke akiwa na nia ya kutaka kutoa mimba kinyume cha sheria akala sumu au kitu kingine cha kudhuru au akatumia nguvu ya namna yoyote au akatumia njia yoyote nyingine iwayo au akaruhusu kutumiwa kwa kitu kama hicho au kufanyiwa kama hivyo, mwananamke huyo atakuwa ametenda kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miaka saba.
IMEANDIKWA NA;
Mwanasheria
Johnson Yesaya Mgelwa (@yesayajm_ )
Wa Jungu la sheria Tanzania.
0758218269