Waandishi wa habari Mkoa wa Njombe wapewa Ubalozi hifadhi ya kitulo

0

Tafadhali tazama picha za matukio mbalimbali ya tour ya waandhi Wa habari Mkoa Wa njomne na soma habari chini.
Picha ni baadhi ya waandishi Wa habari wakiwa nje ya ofisi za Hifadhi ya kitulo wakipiga picha ya kukumbukumbu,miongoni mwao ni Mwenyekiti Wa Njombe Press Club (NPC) Nickson Mahundi Wa pili kutoka Julia.

Waandishi Wa habari wakiwa katika eneo lililojengwa kwa usawa katika sehemu moja wapo katika hifadhi hiyo ambapo unaweza kuuona Mji Wa rujewa eneo lililoko Mkoa Wa Mbeya kwa urahisi zaidi.

Waandishi Wa habari wakiwa katika moja ya gari LA hifadhi ya kitulo ili kufurahia halo ya hewa ya eneo hili baada ya kuwa ndani ya basi kwa muda mrefu,wengine wakirekodi madhari ya eneo hill.

Baadhi ya waandishi Wa habari kutoka kituo cha redio Green FM iliyoko wilayani Makete aliyevaa kodo na aliyechuchumaa wakiwa katika moja ya kibao kinachoelezea umbali kutoka eneo hilo LA mapokezi katika hifadhi na maeneo mengine.

Mwandishi Wa habari Wa mtandao Wa Idawa Online akiwa na Kaimu mhifadhi mkuu Jackson Shirima.

Waandishi Wa habari wakiendelea kuchukua picha za kumbukizi kwamba waliwahi fika hifadhini hapo mwaka 2021.

Waandhi Wa habari wakia katika moja ya maporomoko ya maji baada ya mteremkoa zaidi ya dakika 20-30 hivi hatimaye wakafika kufurahia madhari ya eneo hill katika hifadhi ya kitulo.

Kaimu Mhifadhi mkuu akipata picha na waandishi Wa habari

Wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe Njombe Press Club (NPC) wamefanya ziara ya kutembelea hifadhi ya kitulo iliyopo wilayani Makete Mkoa wa Njombe ikiwa ni sehemu ya kujifunza na kutangaza utalii wa Ndani.

Mapema Disemba 5 2021 wanachama wapatao zaidi ya 35 wameshiriki safari hiyo ya kutangaza utalii kutoka vyombo vya habari mbalimbali vya mkoa wa Njombe na Nje ya Mkoa wa Njombe.

Awali viongozi wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe NPC akiwemo Nickson Mahundi mwenyekiti wa NPC na Katibu wa NPC Hamis Kassapa wamewaeleza waandishi wa habari kuwa Hifadhi ya kitulo ina vivutio vingine hivyo ni nafasi pekee waliopata waandishi hao kwa pamoja kushiriki kutembelea hifadhi hiyo na kujifunza.

'

Waandishi wa habari nawasihi zinapotokea fursa kama hizi za kufanya tour ni vizuri kila mmoja kushiriki kuna mengi yakujifunza,kwa sababu inawezekana peke yako usingeweza kufanya ziara kama hii,huku kuna ndege ambao ni nchi chache sana duniani zinazoweza kuwaona sisi tutawaona sababu ndio miezi yao kuwa nchini Tanzania '
amesema Kassapa.

Baada ya kufika Hifadhini waandishi hao walipokelewa na kaimu mhifadhi mkuu Bw.Jackson Shirima ambaye alieleza kufurahishwa na safari ya waandishi wa habari kufika kutalii na kuwaomba wawe mabalozi wa utalii wa hifadhi hiyo,kisha kuwapa elimu ya mtalii awapo hifadhini ikiwa ni pamoja na kutokupiga kelele hifadhini,kunywa au kuogelea katika maji yaliyoko katika hifadhi hiyo pamoja na kutotupa taka yoyote katika hifadhi hiyo ambayo amesema ni Bustani ya maua.

Miongoni mwa mambo yaliyowavutia wengi ni uwepo wa Maua mbalimbali katika hifadhi hiyo ya kila aina ,uwepo wa zao la Chikanda ambalo linadaiwa kuwa zao la matajiri na linadaiwa kuchangia nguvu za kiume kwa dhana zilizoko miongoni mwa jamii duniani zinazotumia zao hilo la asili na Matunda poli .

Chikanda ikapata kuulizwa maswali baada ya hifadhi hiyo kueleza inaendelea kupambana na wachimba chikanda katika hifadhi hiyo ambapo mmoja ya waongoza watalii alisema

'Chikanda ni mmea unao toa mfano wa kiazi kimoja na kinatumika kwa chakula  umekuwa ukichimbwa sana na watu kwa dhana kuwa unasaidia kuongeza nguvu za kiume na wengine wameweka na dhana kuwa chikana ni chakula cha matajiri'alisema akijibu swali la waandishi wa habari

Waandishi wa habari kutoka mkoa wa Njombe walitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya malazi,sehemu za mapumziko kwa watalii maporomoko ya maji na kuwaona wanyama wengine kama swala jambo ambalo liliwafurahisha wengi katika safari hiyo.

Baada ya safari ya zaidi ya masaa matatu hadi manne katika hifadhi hiyo iliyojaa madhari mazuri na yakuvutia hatimaye utalii ulihitimishwa huku Kaimu Mhifadhi Mkuu Bw.Jackson Shirima akiwatakia safari njema waandishi hao na kuwakumbusha kuendelea kuwa mabalozi wa hifadhi hiyo.

"

Nawaomba muwe mabalozi Wa hifadhi yetu katika Mkoa wa Njombe,naimani kupitia ninyi tutaendelea kupata wageni wengi katika hifadhi yetu"
alisema Shirima

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top