WANAFUNZI 254 WAPATA UJAUZITO WILAYANI SENGEREMA!

0

Wanafunzi wapatao 254 wa shule za msingi na Sekondari Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza wamekatishwa masomo kwa kupatia ujauzito kwa mwaka Kati ya mwaka 2020/21.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa  dawati la Jinsia Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza Insepectar wa Polisi Martha Silvesta alipokuwa akizungumuza na vyombo vya habari Desemba 11 mwaka huu.

Amesema mwaka 2020 lilipotokea janga la ugonjwa wa Uviko 19 wanafunzi wakalazimika kufunga shule  na kurudi nyumbani  wanafunzi wa kike wapatao 168 waligundulika wakiwa na ujauzito huku mwaka 2021 waligundulika wanafunzi wakiwa na ujauzito 86.

Amesema dawati la jinsia wamejipanga kutoa elimu ya ukatili wanaofanyiwa watoto wa kike hasa wa chini wa umri wa Miaka 18 Ili watokomeze jambo hilo.

Martha amesema kitendo cha kumpatia ujauzito mtoto wa kike chini ya miaka 18 ni tendo la ukatili hivyo jamii inatakiwa kuachana na tabia hiyo ambavyo inamdidimiza mtoto wa kikie.

" Mimba hizi zimeripotiwa dawati la jinsia changamoto iliyopo ni wahusika kutokupatikana kwa kuwa wametoroka hivyo jamii inatakiwa kushirikiana na dawati kuhakikisha watu waliofanya vitendo vya ukatili wanachikuwa hatua" amesema Silvesta.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top