Aliyekatishwa masomo arejea shuleni na mtoto kutimiza ndoto ya kielimu.

0

 Esnath Gideon (19) akiwa darasani na mwanaye mwenye umri wa miezi minne kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan kuruhusu waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali kurejea shule.


"Sina mtu wa kumwachia mtoto nyumbani, na uwezo wa kumlipa mtu sina, ila nashukuru nilivyokuja shule, waliniruhusu kuingia na mtoto darasani," anasema Esnath.

Esnath alipewa ujauzito na kijana aliyekutana nae siku moja wakiwa safarini bila kumfahamu kwa kina. Ilikwua ni mwaka jana akiwa kidato cha nne. Miezi mitano baada ya kugundulika shuleni alilazimishwa kukatisha masomo yake. Huu ulikuwa ni ukurasa mpya katika maisha yake.

"Nilijisikia vibaya sana nilipogundua nina ujauzito. Sikuona mbele wala nyumba. Niliona giza tu mbele yangu. Nilipoteza mwelekeo kabisa. Ndoto zangu zote zilikufa. Sikufikiria kama kuna siku nitarudi tena shuleni," anasema Esnath.

Hata hivyo, hali hii haikuishia kwa Esnath pekee, bali familia yake yote ilijawa na simanzi baada ya kuona binti yao amekatisha masomo

Binti huyo Amesema alipoteza matumaini alipopata ujauzito akiwa kidato cha nne, lakini sasa anataka kusoma kwa bidii awe Mwanasheria.

📸 Story via BBC
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top