MKE, MUME WASHIKILIWA KWA MAUAJI MWANZA

0

 Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikiliwa watu  watano wakiwemo mume na mke wake kwa tuhuma za mauaji ya wanawake watatu wa familia moja wakazi wa mtaa wa Mecco Kusini jijini Mwanza.

Watu hao wa familia moja waliouawa Januari 18, 2022 ni Marry Charles (42) mfanyabiashara mkazi wa Mecco, Jenifa Fred (22) mkulima ambaye ni mtoto wa marehemu, pamoja na mfanyakazi wao wa ndani, Monica Jonas (19) na waliuawa kwa kukatwa mapanga na miili yao kutupwa kwenye Bonde la mto Jellys uliopo Buzuruga, Manispaa ya Ilemela.

SOMA HII; Askari Polisi wanandoa wauana kwa risasi 

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ramadhani Ng’anzi amebainisha kuwa sababu ya mauaji hayo ni mgogoro wa kibiashara.


Aidha Kamanda Ramadhan Ng’anzi amesema marehemu alikuwa akijishughulisha na biashara ya kuuza nafaka na kwamba alikuwa akiitumia familia ya watuhumiwa kuagiza mzigo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.


Inadaiwa mara ya mwisho marehemu alimpa mmoja wa watuhumiwa kiasi cha fedha ambacho hakijajulikana kwa ajili ya kumuagizia mzigo, matokeo yake mzigo haukuletewa na katika kudaiana ndipo mtuhumiwa huyo wa kwanza akishirikiana na wenzake aliweza kwenda kufanya mauaji hayo,” amesema Kamanda Ng’anzi.


Kamanda Ng’anzi amesema pia watuhumiwa hao walikutwa na silaha aina ya panga iliyotumika kwenye mauaji hayo ambayo ipo chini ya uangalizi wa jeshi la polisi. 

 

Marehemu Marry ameacha mtoto wa mwaka mmoja  na binti yake  Jenifa ameacha mtoto wa mwezi mmoja  na kwa sasa  watoto hao wapo chini ya uangalizi maalumu  huku  Miili ya marehemu ikizikwa kijijini kwao Bomani  wilaya Sengerema usiku  wa Januari 21, 2022.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top