Atuhumiwa kumuua baba mkwe kwa jembe!

0

 Mkuu wa Wilaya ya Siha na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Thomas Apson, amethibitisha kupokea taarifa kuhusu mauaji hayo yaliyotokea katika Kijiji cha Mlangoni, Kata ya Gararagua.

“Ni kweli hayo mauaji yalitokea jana (juzi) jioni baada ya Joyce Siao (45), ambaye ni mke wa mtoto wa mzee Godson Moshi (80), kumpiga jembe kichwani baba mkwe wake.


Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mlangoni, Swalehe Mohamed, alisema lilitokea juzi majira ya saa 1:30 jioni nyumbani kwao.


“Huyu mwali (Joyce) alikuwa akiishi na baba mkwe wake (Godson) baada ya mume wake kufariki dunia miaka kadhaa iliyopita. Kabla ya kuchukua uamuzi wa kumpiga na jembe kichwani, mtuhumiwa wa mauaji hayo alikuwa amehitilafiana na baba mkwe wake.


“Sasa baada ya kutekeleza dhamira yake, majirani walisikia kelele na kukimbilia katika nyumba hiyo na kumkuta baba mkwe wake akiwa ameanguka. Walimchukua baba huyo na kumpeleka hospitali ya wilaya kwa ajili ya kupatiwa matibabu, lakini kabla ya kupatiwa matibabu, alifariki dunia,"

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top