HATIMA KESI YA MBOWE NA WENZAKE KUTOLEWA IJUMAA!

0

 Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imesema Ijumaa Februari 18, 2022 itatoa uamuzi iwapo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wana kesi ya kujibu au la katika kesi ya ugaidi inayowakabili.
Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo amesema hayo leo Jumanne Februari 15, 2022 baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahaka kuwa wamefunga kesi hiyo kwa shahidi wa 13 kuhitimisha ushahidi wake.

Shahidi huyo wa 13 wa upande wa mashtaka ambaye ni Mkaguzi wa Polisi, kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Kipolisi Temeke, Tumaini Swila amemaliza kutoa ushahidi baada ya kuhojiwa maswali ya dodoso na upande wa utetezi.

Baada ya shahidi huyo kuhitimisha ushahidi wake, Wakili wa Serikali Robert Kidando aliiambia Mahakama kuwa wamefunga ushahidi na kuiomba mahakama ione kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu.

“Baada ya ushahidi wa shahidi huyu wa kumi na tatu tunaialika Mahakama yako chini ya kifungu 41 (1) cha sheria ya Uhujumu Uchumi ione washtakiwa wote wanne wana kesi ya kujibu hivyo hatua nyingine kwaajili ya kujitetea ifuate kwa upande wetu tunafunga kesi hii” amesema Wakili Kidando

Hata hivyo, baada ya kutoa ombe hilo, upande wa utetezi kupitia Wakili Peter Kibatala umeomba kupewa nafasi ya kufanya mawasiliano ya mdomo pamoja na kupewa mwenendoi wa kesi.

“Baada ya upande wa mashtaka kufunga kupitia kifungu hicho cha 41 tunaomba mahakama hii itupe nafasi ya kufanya mawasilisho ya mwisho Lakini pia tuna maombi mawili ombi la kwanza Mahakama itupe mwenendo wa kesi lakini pili tupewe nafasi ya kufanya mawasilisho ya mwisho oral” amesema Kibatala.

Akijibu hoja hizo, Jaji Joachim Tiganga amesema Mahakama hiyo itatoa uamuzi Ijumaa wa kuwa washtakiwa hao wana kesi ya kujibu au la. 

“Baada ya kusikiliza na kupitia hoja za pande zote mbili na kuzingatia kifungu cha 41 cha Sheria ya Uhujumu Uchumi, Mahakama hii itatoa uamuzi Februari 18, 2022 kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la saa nane mchana na washtakiwa mtaaendelea kubaki chini ya uangalizi wa magereza” amesema Jaji Tiganga .

CC: Mwananchi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top