Waandishi wa habari wametakiwa kutambua kuwa uandishi wa habari ni taaluma na wanapaswa kufuata misingi ya uandishi kwa kuandika habari katika ubora.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania TEF Deodatusi Balile katika washa ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi katika uandishi Wa habari katika uwanda wa kiraia.
Balile amesema kuwa waandishi wanapaswa kufuata misingi mikuu mitatu ikiwemo Uhuru wa vyombo vya habari,uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kupata habari.
Kwa upande wake Godliver Shiyo mratibu wa mradi wa boresha habari Kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajea uwezo waandishi wa namna ya kuandika Makala,kutoa taarifa zinazolenga kuelimisha umma juu ya haki katika uwanda wa kiraia ikijumuisha haki ya kupata habari,haki ya kujieleza na haki ya Uhuru wa vyombo vya habari
Kwa upande wao waandishi wa habari akiwemo Brighter nyoni kutoka icefm Njombe na Titho Sovella kutoka Keyfm Ruvuma wamesema kuwa kupitia mafunzo hayo wataenda kuwa sehemu ya mabadiliko katika uandishi wao wa habari kuhusu waandishi na jamii.
Jumla ya wandishi wa habari 60 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wameshiriki mafunzo hayo ya Siku mbili ili kuwajengea uwezo yaliyofanyika jijini Dodoma.
TAZAMA VIDEO YA MAFUNZO HAPA