Imelezwa kuwa wanawake wilayani Makete Mkoani Njombe wamezidi kuelimika katika suala la umiliki wa ardhi kwa kuwa na hati miliki zao.
DC MAKETE JUMA SWEDA.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Kiwilaya katika kata ya Tandala mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya Mh.Juma Sweda amesema kuwa ni lazima kuwe na usawa katika umiliki mali na ardhi pamoja na elimu.
Pia amewataka wazazi na walezi wilayani Makete kushirikiana na ofisi yake katika kufichua matukio ya ukatili yanayofanyika katika jamii.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Makete Jackline Mroso ameelezea lengo la kuwepo kwa maadhimisho hayo huku akiwakumbusha wakinamama kutimiza wajibu katika maelezi ya familia.
Katika risala yao wanawake wa kata ya Tandala wamesema licha ya jitihada nyingi katika kuwainua bado kuna changamoto ikiwemo kukosekana kwa elimu ya ujasiriamali pamoja na mikopo kutokidhi mahitaji ya wanawake.
TAZAMA VIDEO YA DC MAKETE AKIWAONYA WANAUME KUWAPIGA WAKE ZAO!.