Akizungumza mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Luwizo 23 amesema awali alimpenda mmoja wao aitwaye Natalie ambaye walikutana kupitia mtandao Wa Facebook,na siku walipopanga kukutana kwa lengo la kujuana na kupeana penzi nyumbani kwa Natalie alishangaa kupokewa na Wanawake watatu wanaofanana akiwemo Nadege na Natasha.
Wawili hao walidai kumpenda pia Ingawa hakuwa na habari, Luwizo alikuwa akikaribishwa na mmoja wa mapacha watatu kila alipotembelea nyumbani kwa Natalie kutoka tangu waingie kwenye mahusiano yao.
Luwizo anasema alipoanga siku ya kukutana kwao ili kufanyanya mazungumzo ya mwisho ya kukubaliana kuoana alipofika nyumbani ndipo aliposhtuka kupokewa na Wanawake watatu hali ilimshtua sana kiasi cha kukaribia kuzimia kwa mushtuko.
Niliwauliza kati yenu nyote, Natalie ni nani? Waliniambia nimekutana nao wote siku tofauti nilizotembelea," alisema. “Nilichanganyikiwa kwani nilipanga kumuoa Natalie lakini kilichonichanganya ni kwamba singeweza kuoa msichana mmoja na kuwaacha wawili hao! Dada hao walisema walikuwa na amani ya kuolewa naye kwa sababu wamekuwa na uhusiano wa karibu tangu utotoni.
"Mwanzoni, tulipomwambia kwamba lazima atuoe sote alishtuka ,Lakini kwa sababu tayari alikuwa ametupenda sote, hakuna kitu ambacho kiliweza kuzuia mipango yetu kwa vile tulikuwa tukimpenda," Natalie alisema.
"Ingawa watu wanaona kuwa haiwezekani kwa wanawake watatu kugawana mume mmoja, lakini kwetu, kugawana kila kitu imekuwa maisha yetu tangu utoto.
" Wazazi wa Luwizo, hata hivyo, walipinga uamuzi wake na wakajiondoa kwenye sherehe za harusi.
"Lazima upoteze kitu ili kupata kingine,Kwa kuongezea, mtu ana mapendeleo yao na njia yao ya kufanya mambo hata kama wazazi wamenisusia kikubwa nimepata familia." Aliongeza:
"Nina furaha kuoa watoto watatu bila kujali wengine wanafikiria nini Upendo hauna kikomo.”
TAZAMA VIDEO YA HARUSI YAO HAPA AOA MAPACHA WATATU.