Na Bilgither Nyoni
Mkoa wa Njombe umeandikisha jumla ya wanafunzi 24,217 kuanza darasa la kwanza kwa mwaka wa masomo 2022 sawa na asilimia 103 Ukiwa Umevuka lengo lililokuwa limewekwa huku darasa la awali ukiwa wameandikisha wanafunzi 23,978 sawa na asilimia 99 .
Akizungumza na Ice Fm Afisa Elimu Mkoa wa Njombe MWL NELASI MULUNGU Amesema kati ya walioandikishwa wanafunzi wa Darasa la kwanza wavulana ni 12,347 huku wasichana wakiwa 11,874.
"tulitegemea kuandikishaji wanafunzi wa darasa la kwanza 23,499 lakini mpaka sasa tumeweza kuvuka lengo la uandikishaji ambapo tumeandikisha wanafunzi 24,217 kwa hiyo asimilimia ya uandikishaji ni 103,kwa darasa la awali tulitegemea 24,031 lakini mpaka sasa tumeandiksha 23,978 hiyo ni sawasawa na asilimia 99"Alisema
Aidha Afisa Elimu huyo Amesema zoezi la uandikishaji litamalizika Marchi 31 mwaka huu hivyo amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shule kuanzia darasa la awali, la kwanza na kidato cha kwanza kabla ya kuufungwa kwa zoezi la uandikishwaji.
"kwa kweli uandikishaji ni mzuri na zoezi hili zima tunategemea kuisha tarehe 31 mwezi huu wa tatu"alisema
Kufuatia uandikishaji huo Afisa Taaluma msingi katika halmashauri ya mji wa Makambako BHOKE BIRORE Aamesema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanawafundisha vizuri wanafunzi kwa utaratibu uliowekwa na serikali Na kutatua changamoto zilizopo shuleni.
"kwa hiyo tukiandikisha watoto wengi hiyo ndiyo furaha yetu maana hiyo ndiyo kazi yetu kwa hiyo tukiandikisha wengi tunajipanga pia kuhakikisha kwamba tunawahudumia vizuri kwa sababu ndiyo kazi yetu na ndio wateja wetu ndo wanaotuweka mjini na tumejipanga tunahakikisha walimu wetu wanafundisha vizuri kwa kufata utaratibu zote za kufundisha na sisi kama ofisi tunafatilia kuona nini kimefanyika"Alisema
Nao baadhi ya walimu wakuu wa shule za msingi mjini makambako,Akiwemo mwl maria msigwa wa shule ya msingi Makambako ,mwlErick mtweve wa usetule na mwl frowin Mgeni wa mwembetogwa B wamesema kuwa kuwepo kwa elimu bila malipo,chakula kutolewa shuleni pamoja na kamati za shule kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shule kumechangia kwa kiasi kukubwa kuvuka lengo la uandishaji wa darasa la kwanza.