NJOMBE; SERIKALI YATAKIWA KUHAKIKISHA CHANJO ZINAZOHITAJI KWA WATOTO ZINATOSHELEZA!

0

 Na,Bilgither Nyoni

Licha ya serikali kupitia wizara ya afya kuja na kampeni ya utoaji chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya maika mitano ili kukabiliana na ugonjwa wa kupoonza unaosababisha ulemavu wa kudumu na kifo lakini Imetakiwa kuhakikisha chanjo zote zinazowahusu watoto wadogo zinapatikana kwa wingi kwenye vituo vya afya ili kulinda afya ya mtoto.

Akizungumza katika zoezi la uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya polio ambayo imezinduliwa katika kituo cha afya makambako,Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako Hanana Mfikwa amesema licha ya chanjo ya polio kutolewa kwa sasa bado wizara inatakiwa kuhakikisha chanjo zote ambazo watoto wanatakiwa kuzipata, zinapatika katika vituo vote vya afya ili kuepuka  na magonjwa mengine yanayoweza kuwapata.


Nae Msimamizi wa chanjo kutoka wizara ya afya kitaifa Dkt Monica Billa amewataka wazazi na walezi kujijengea tabia ya kuchunguza afya za watoto wao ili kubaini kama wanadalili za ugonjwa wa polio ili waweze kupatiwa matibabu.


Mratibu wa chanjo katika halmashauri ya mji wa makambako Tindichebwa Mazala amesema mara baada ya uzinduzi wa chanjo hiyo ya polio,wataalam wanapita nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha watoto wote wanapatiwa chanjo hiyo na kufafanua kuwa chanjo hiyo itatolewa na kwa watoto wote waliopo kwenye vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.


Nao baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamepatiwa chanjo hiyo,wameiomba jamii kushirikiana na wataalam wa afya ili kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo hiyo ili kuwakinga na ugonjwa wa kuupoanza.


Kampeni ya utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto chini ya miaka mitano itatolewa hadi tarehe 27 mwezi marchi na itahusisha mikoa minne ikiwemo mkoa wa Njombe,Ruvuma,Mbeya na Songwe lengo likiwa ni kukabiliana na ugonjwa wa kupoonza ambao umeripotiwa nchi jirani ya malawi hivi karibuni.

KAMA HUKUTAZAMA VIDEO HII BOFYA SASA KUTAZAMA SASA!


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top