Serikali ya wilaya ya Makete imesema itaendelea kutoa ushirikiano kwa Shirika la Kudhihirisha Uzalendo MAPAO kwani wamekuwa wakisaidia serikali kuelimisha jamii juu ya masuala ya sheria.
Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi Pamoja wadau wa msaada wa kisheria katika zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Ofisi za Shirika hilo lililopo wilayani Makete mkoani Njombe.
Wakitoa salamu kwa washiriki wa zoezi hilo akiwemo Hakimu mkaazi wa wilaya ya Makete Dennis Mujwahuzi na Msafiri Lubega wamesema wananchi wengi wamekosa elimu ya sheria ikiwemo kwenye mirathi na migogoro ya ardhi.
Akizoma Risala kwa Mgeni Rasmi Mratibu wa shirika la kudhihirisha uzalendo MAPAO Bi Neema Sanga amesema ujenzi wa ofisi hizo unatarajiwa kugharimu zaidi ya milioni 46 mpaka kukamilika kwake.
Apolo Laizer ni mwansheria wa wilaya ya Makete akimwakilisha Mgeni Rasmi ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Makete amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini shughuli zinazofanywa na shirika hilo na kwamba serikali itaendela kutoa ushirikiano.
BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO HAPA YA TUKIO ZIMA!👇