
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah
**
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa vifo vya
watu 8 na 19 kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya Coaster T 287 CCY
mali ya kanisa Katholiki Njombe iliyogongana na lori la makaa ya mawe.
Watu
hao ni miongoni mwa Umoja wa vijana kanisa katoliki Jimbo la Njombe
(UVIKANJO) ambao walikwenda kuwatembelea watoto yatima katika kituo cha
Ibumila wilayani Njombe.

Orodha ya majina ya waliofariki kwenye ajali
Ajali ilitokea jana majira ya jioni katika eneo la Igima wilayani Wanging’ombe Barabara kuu (TANROADS) kuelekea mkoa wa Ruvuma.
Aidha
amesema majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mji
wa Njombe Kibena pamoja na hospitali ya rufaa ya mkoa huo.