Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linamshikilia Mama mmoja Mwamba Thomas Msukuma (37) kwa kosa la kuchomwa na maji ya moto mtoto wake India Itito (4) kwenye Mikono yake miwili kwa kile kilichodaiwa mtoto huyo kuiba tambi ambazo ziliandaliwa kwa ajili ya chakula cha Mchana.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani humo ACP Shadrack Masija, imeeleza kuwa tukio hilo la kikatili limetokea Tarehe 22/04/2022 majira ya Saa 10:00 jioni katika Mtaa wa Kidinda Kata ya Bariadi Tarafa ya Ntunzu Wilaya ya Bariadi na Mkoa Simiyu.
“ Kwa sasa mtoto amelazwa Hospatali ya Wilaya ya Bariadi na anaendelea na Matibabu, mara baada kukamilisha upelelezi wa shauri hilo jalada litafikishwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Simiyu kwa hatua za kisheria zaidi,” alisema Masija.