Taarifa iliyoufikia mtandao huu kutoka chama cha walimu Tanzania CWT wilaya ya Makete mkoani Njombe ni kwamba walimu wafuatao wanapaswa kufika kwa mwajiri haraka iwezekano jumatatu mei 2 2022.
1- WALIMU WALIOPANDA CHEO 2017 NA APRIL, 2018
2-WALIMU WALIOAJIRIWA 2016 KAMA WAPO WAPELEKE BARUA ZA KUPANDA CHEO HARAKA IWEZEKANAVYO JUMATATU YA TAREHE 02 MEI 2022 BILA KUKOSA.
Mwl Betson Kwama amesema kutokana Na hali hewa na miundombinu ya wilaya ya Makete ameshauri walimu hao kama wapo kundi sehemu/ukanda mmoja wanaweza kuzikusanya barua kisha kuzituma kupitia mmoja wao ili kuokoa garama na muda.
Aidha ameshauri mwllalimu atakaye pata ujumbe huu kupitia redio au mtandao huu amjulishe mwingine ili taarifa ziwafikie wahitaji.
TUNAOMBA SHARE HABARI HII IWAFIKIE WALIMU HUSIKA HARAKA IWEZEKANO AU MJUZE JUU YA TAARIFA HII.