Mtoto aliyedaiwa kufa kwa njaa afukuliwa

0

 Mtoto Salah Jackson (5) aliyezikwa na mama yake kimyakimya usiku baada ya kudaiwa kufa njaa, leo amezikwa rasmi katika kijiji cha Makiwaru wilayani hapa Mkoa wa Kilimanjaro.


Mtoto huyo alifariki dunia Aprili 21 na kisha mama yake aitwaye Rebecca Siowi (30) kumzika kimya kimya katika nyumba ya mama yake baada ya mume wake kumtelekeza akiwa na watoto watano.

Kutokana na tukio hilo la mama kumzika mwanaye mwenyewe usiku wa manane liliwaibua Jeshi la polisi mkoani hapa ambapo mwili wa mtoto huyo ulifukuliwa Aprili 22, kwa ajili ya kwenda kuufanyia uchunguzi wa kina kujua uhalali wa kifo cha mtoto huyo.

Hata hivyo, alipotafutwa Kamanda wa polisi Mkoani hapa, Simon Maigwa alisema baada ya kuufukua mwili wa mtoto huyo ulipelekwa hospitali kwa ajili ya kuufanyia uchunguzi ambapo mtoto huyo alibainika kuwa alikufa kwa njaa kwa mujibu wa majibu ya madaktari.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top