JESHI
la Polisi mkoani Shinyanga, linamshikilia kijana Mwandu Shija (32)
mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga, kwa tuhuma za kumuua baba yake
mzazi Shija Robert (55) kwa madai ya kumfumania akiwa amelala na mkewake
kitandani.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, alisema wakati kijana huyo aliporudi nyumbani ndipo akamfumania baba yake akiwa amelala na mkewake na kuanza kumshambulia.
Alisema
wakati kijana huyo akiendelea kumshambulia Baba yake na kipande cha
kuni sehemu mbalimbali za mwili wake, ndipo alipompiga sehemu mbaya na
kusababisha mauaji.
“Chanzo
cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi, baada ya marehemu kukutwa akiwa
amelala kitanda kimoja na mke wa mtuhumiwa,”alisema Kyando.
“Mwili
wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari na kuhifadhiwa katika
Hospitali ya rufani mkoani Shinyanga, ukisubili kukabidhiwa kwa
wanandugu kwa ajili ya mazishi,”aliongeza.
Aidha,
alisema Jeshi la Polisi mkoani humo bado linaendelea na uchunguzi wa
tukio hilo, na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa
hatua zaidi za kisheria.
Na;Marco Maduhu.
TAZAMA VIDEO HII YA MBUNGE JIMBO LA MAKETE ISIKUPITE