2:Kwa masharti yafuatayo:
(i) Wafungwa wote wapunguziwe robo (1/4) ya vifungo vyao baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu (1/3) linalotolewa chini ya Kifungu cha 49 (1) cha Sheria ya Magereza, Sura ya 58.
Wafungwa hao sharti wawe wametumikia robo (1/4) ya vifungo vyao na wawe wameingia gerezani kabla ya tarehe 26 Februari, 2022 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika sharti la 2(i–ii);
(ii) Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu ambao wametumikia robo (1/4) ya vifungo vyao na wapo kwenye Terminal Stage, ugonjwa huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya;
(iii) Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi ambao wametumikia robo (14) ya vifungo vyao. Umri huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya;
(iv) Wafungwa wa kike walioingia gerezani wakiwa na watoto wanaonyonya, wasionyonya na wajawazito ambao wametumikia robo (1/4) ya vifungo vyao;
(V) Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (physical disability and mental disability) ambao wametumikia robo (1/4) ya vifungo vyao. Ulemavu huo uthibitishwe na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya;
(vi) Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kuwekwa kizuizini (Under President’s Pleasure) ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka kumi (10) na kuendelea;
(vii) Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka thelathini (30) na kuendelea;
(viii) Wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha gerezani ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka ishirini (20) na kuendelea;
(ix) Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya kujaribu kuua .
SOMA ZAIDI TAARIFA HII HAPO CHINI!