
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 28, 2022, Kamanda wa Kanda hiyo Jumanne Muliro amesema vijana wengi waliokamatwa umri wao unaanzia miaka 13 hadi 21.
Amesema baada ya kuhojiwa, vijana hao wamekiri kuhusika na matukio hayo na wamendelea kuisaidia Polisi kuhakikisha wenzao wanaotoka maeneo mbalimbali waliohusika na matukio hayo wanakamatwa.
“Vijana hao wamekuwa wakitumia mapanga kuwajeruhi watu na Jeshi la Polisi tuliongea na wenyeviti wa mtaa na mabalozi tumekubaliana hali hiyo haiwezi kuendelea lazima watapambana na mkono wa chuma vijana wanaojihusisha na matukio hayoa” amesema
Amesema mbali na vijana hao kuiba mali za watu katika tukio hilo la Chanika waliwajeruhi watu 23 kwa kuwakata mapanga sehemu mbalimbali na wengi wao wapo hospitali wakiendelea na matibabu.
"vijana hao ni wadogo wamekamatwa na wameongea mambo mengi naamini kulingana na uchunguzi tunaendelea kuufanya tutafika pazuri,"amesema