WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa amesema pamoja na kuwepo kwa ongezeko la wanafunzi waliojiunga na Kidato cha tano, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi kwa mwaka 2022, jumla ya wanafunzi 14,254 wakiwemo wasichana 3,901 na wavulana 10,353 wamekosa nafasi.
Akizungumza leo Mei 12, 2022 Bashungwa amesema, kati yao wanafunzi 12,876 wana sifa ya kujiunga na kidato cha tano na hali hiyo imechangiwa na ufinyu wa nafasi.
“Hali hii imetokana na ongezeko kubwa la wanafunzi waliofaulu na waliokuwa na sifa ya kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi pamoja na ufinyu wa nafasi za Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi (NACTVET).
"Wanafunzi hao wanatarajiwa kujiunga na kidato cha tano katika awamu ya pili baada ya ukamilishaji wa baadhi ya miundombinu ya shule na vyuo,"amesema.