Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Kamishna Msadizi wa Polisi Daniel Shillah amethibitisha kutokea kwa Ajali ya Gari iliyopelekea kifo cha mtu mmoja na mmoja kujeruhiwa katika Barabara ya Nungwi ndani ya Mkoa huo Visiwani Zanzibar
Kamanda Shillah amesema ajali hiyo imetokea leo (Jumatatu 02 Mei, 2022) huko katika eneo la Kendwa kuelekea kidoti ambapo Dereva wa Gari aina ya Hilux yenye namba za Usajili Z306 GQ aliyefahamika kwa jina la Abdul Rahman Rashid Juma (27) ilimshinda kukunja kona na kuacha njia na kugonga miti
Amesema Dereva wa gari hiyo na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Yunus Mohammed Said (23)walifikishwa katika Hospitali ya Kivunge na hadi sasa Dereva amepoteza maisha na mwenzake akiendelea na matibabu.