AMUUA MKEWE KWA KUZIDISHA CHUMVI KWENYE CHAKULA

0

Polisi nchini India wamemkamata mwanaume mwenye umri wa miaka 46 ambaye anadaiwa kumuua mkewe kwa sababu kifungua kinywa chake kilikuwa na chumvi nyingi.

''Nikesh Ghag, karani wa benki huko Thane, karibu na mji wa magharibi wa Mumbai, alimnyonga mke wake mwenye umri wa miaka 40 kwa hasira kwa sababu chakula kinachofahamika kama khichdi ya sabudana alichokuwa anamuandalia kilikuwa na chumvi nyingi,'' afisa wa polisi Milind Desai, alisema

Mtoto wa wanandoa hao mwenye umri wa miaka 12, ambaye alishuhudia uhalifu huo, aliwaambia polisi kwamba baba yake alimfuata mama yake, Nirmala, chumbani akilalamikia chumvi iliyopitiliza kwenye chakula na kuanza kumpiga.

Baada ya Bw Ghag kutoka nje ya nyumba kwa mtoto huyo aliwaita bibi yake mzaa mama na mjomba wake.

''Kufika eneo la tukio, familia yake ilimkuta katika hali mbaya na kulazimika kumkimbiza hospitalini, lakini wakati huo alikuwa tayari amefariki,'' Bw Desai alisema.

Baadaye mshtakiwa alijisalimisha katika kituo cha polisi, ambapo aliwaambia maafisa kuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu.

Mauaji ya mwanamke na mumewe, yaliyochochewa na ugomvi juu ya chakula, mara kwa mara yanagonga vichwa vya habari nchini India.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top