Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 24 ambaye alilipwa kimakosa mamilioni ya pesa ya Japani tayari amepoteza pesa hizo baada ya kucheza kamari mtandaoni.
Mwanamume huyo alipokea yen milioni 46.3 sawa na dola $357,400 (£287,000) kwenye akaunti yake ya benki zikiwa ni pesa kutoka mfuko wa misaada ya Covid ambayo ilipaswa kugawanywa kwa watu 463.
Hapo awali alisema atashirikiana na viongozi, lakini hakuonekana.
Mji wa kusini wa Abu katika Mkoa wa Yamaguchi nchini Japan unamshtaki mwanamume huyo na pia wamechukulia hatua hiyo kama kitendo cha uhalifu.
Pesa hizo zilipaswa kulipwa kwa kaya 463 za kipato cha chini ambapo kila kaya ilipaswa kupokea yen 100,000 sawa na dola $ 770 (£ 620) kama sehemu ya mpango wa serikali wa kupunguza mkali ya kifedha yaliyosababishwa na janga hilo.
Lakini tarehe 8 Aprili, pesa zote yen 46.3m ziliwekwa kwa bahati mbaya kwenye akaunti ya kibinafsi ya benki.
Uchunguzi umegundua kuwa alitoa yen 600,000 kila siku kwa takribani wiki mbili, vyombo vya habari vya ndani vinaripoti