BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI

0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa ametoa mwezi mmoja  kwa Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es salaam kufanya upembuzi yakinifu wa barabara Suca - Golani katika halmashauri ya Manspaa ya Ubungo yenye urefu wa kilometa 7.5 ili itengewe bajeti na kujengwa kwa kiwango cha lami.

Bashungwa ametoa maagizo hayo  kwa Meneja huyo Mhandisi Geofrey Mkinga wakati wa ziara katika  Halmashauri ya Manispaa ya  Ubungo  kukagua barabara ya Suca - Gorani inayohudumia kata mbili ya Saranga (Jimbo la Kibamba) na Kata ya Kimara (Jimbo la Ubungo).

Amesema baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasaan kusikia kilio cha muda mrefu cha mawasiliano barabara hiyo amemuagiza kufika katika eneo hilo na kuhakikisha anatatua kero hiyo ya wananchi.

Bashungwa amemuagia Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kupitia asilimi 60 ya mapato ya ndani inayotengwa kutekeleza miradi ya maendeleo na asilimi 10  kati ya hiyo inayotengwa kwa ajili ya barabara kulingana na Mwongozo wa Ofisi ya Rais TAMISEMI atenge fedha ambazo atashirikiana na TARURA ili kujenga barabara hiyo.

Aidha, Bashungwa amesema Serikali ya awamu ya sita itahakisha inatatua kero za Wananchi wote bila kujali mijini au vijijini ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapindunzi.

Vile vile, Ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikao kwa timu itayokuwa inafanya upembuzi yakinifu ili kwakamilishe kazi hiyo kwa wakati ya kupata BOQ ili Serikali iweze kuleta fedha za kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top