BREAKING NEWS; SABAYA ASHINDA KESI MAHAKAMA YAMUACHIA HURU.

0

Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha imemuachia huru aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamekata rufaa ya kupinga kuhukumiwa miaka 30 kwenda jela kila mmoja kwasababu mbalimbali kwakuwa Mrufani namba mbili Silvester Nyegu na namba tatu Daniel Mbura hawakupewa haki ya kumhoji Shahidi namba mbili wa Jamhuri na kutokufanya hivyo kunawanyima haki yao msingi.

Jaji aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo, Ezedekia Kisanya amesema kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo ikiwemo kutofautiana kwa mashahidi na kuufanya ushahidi kuwa batili.

Jaji amesema watakuwa huru endapo watakuwa hawana kesi nyingine kwenye Mahakama yoyote.

SOMA HII;Wazazi saidieni serikali kuibua vipaji vya watoto walemavu

Mbali na Sabaya waomba rufaa wengine ni Sylvester Nyegu na Daniel Mbura ambao tayari wamefika mahakamani hapo kusikiliza rufaa inayosikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Sedekia Kisanya.


Leo Mei 6,2022 Sabaya na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo saa 3:30 asubuhi huku ulinzi ukiendelea kuimarisha kwenye viwanja vya mahakama.


Rufaa hiyo ya jinai namba 129/2021 imeletwa na Sabaya na wenzake hao wakipinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.


Katika rufaa hiyo waomba rufaa hao wanawakilishwa na mawakili Majura Magafu, Moses Mahuna, Fauzia Mustafa, Sylvster Kahunduka, Edmund Ngemela na Fridolin Bwemelo ambao kwa pamoja walipinga hoja za wajibu rufaa na kuomba mahakama iridhie hoja zao 14 za rufaa na kuwaachia wateja wao huru.


Upande wa Jamhuri (wajibu rufaa) uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali waandamizi Ofmedy Mtenga, Verediana Mlenza na Baraka Mgaya ambao, wanapinga hoja za mawakili wa waomba rufaa na kuiomba mahakama itupilie mbali rufaa hiyo.

Awali Oktoba 15, 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo aliwahukumu Sabaya na wenzake wawili kifungo cha miaka 30 kila mmoja, baada ya kuwatia hatiani kwa makosa matatu ikiwamo unyang'anyi wa kutumia silaha.


Wakati akitoa hukumu hiyo, Hakimu Amworo alisema kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa mahakamani, aliridhika washitakiwa hao walimpora Numan Jasin, Bakari Msangi na Ramadhan Rashid.


Hata hivyo, alisema ushahidi ulionyesha kuwa walipowavamia Numan na Ramadhan walitumia nguvu sio silaha lakini, walitenda kosa la unyang'anyi wa makundi na Jamhuri kuthibitisha kosa hilo walipomvamia Msangi walitumia silaha.


Wakati Mahakama Kuu ikitarajiwa kutoa hukumu hiyo leo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha nayo imepanga Mei 31, 2022 kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Sabaya na wenzake sita.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top