Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema polisi imefanikiwa kumpata diwani wa Kawe (CCM), Mutta Rwakatare aliyekuwa akitafutwa na ndugu zake kuanzia Februari mwaka huu.
![]() |
PICHA KUTOKA MAKTABA |
Hivi karibuni Meya wa Kinondoni, Songoro
Mnyonge akiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani aliviomba vyombo vya dola,
wanahabari kusaidia kumtafuta diwani huyo ambaye ni mtoto wa marehemu Dk
Getrude Rwakatare.
“Tunamtafuta diwani wetu wa Kata ya Kawe hatujamuona
muda mrefu, nyumbani hayupo, ofisini hayupo, kwenye chama hayupo, taarifa
tunaambiwa amefichwa sasa sijui nani kamficha. Tunamtaka huyo aliyemficha
diwani amuachie kwasababu anamnyima nafasi ya kuwatumikia wananchi amuachie na
vyombo vya dola mtusaidie” alisema Mnyonge.
SOMA HII: SABABU ZA WANAWAKE KUBRID DAMU NYINGI NA MUDA MREFU.
Lakini leo Jumanne Mei 24, 2022 wakati
akizungumza na wanahabari, Kamanda Muliro amesema baada ya uchunguzi wa polisi
walifanikiwa kumpata Mutta (43) Mei 23 maeneo ya Tabata akiwa katika nyumba ya
mwanamke mmoja aitwaye Ashura ambaye amedai ni rafiki yake wa siku nyingi.
Kamanda Muliro alisema, “alifika (Mutta) kwa
Ashura Mei 19 mwaka huu akiwa katika hali ya ulevi uliopindukia.
“Kutokana na mazingira ambayo diwani huyo amekutwa nayo na maombi yaliyotolewa na ndugu kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya matibabu, pia walitoa kumbukumbu za nyuma za mwenendo na tabia za Mutta polisi limemkabidhi kwa ndugu zake kwa ajili ya matibabu na tiba za kisaikolojia,” amesema Muliro.
SOMA HII: SABABU ZA WANAWAKE KUBRID DAMU NYINGI NA MUDA MREFU.