DIWANI WA KATA YA BULONGWA AKATAA KUSHIRIKI UJENZI WA BWENI LA WANAFUNZI.

0

Diwani wa Kata ya Bulongwa Mh. Benayo Luvanda amesema hawezi kushiriki ujenzi wa bweni la Wavulana shule ya Sekondari Usililo Kata ya Luwumbu kwa kuwa Bulongwa nao wapo kwenye maandalizi ya kujenga shule yao ya Kata.

Ameyasema hayo alipozungumza na Kitulo FM kuhusu uwepo wa taarifa za wananchi wa Kata ya Bulongwa kutoshiriki nguvu kazi kwenye ujenzi wa Sekondari ya Usililo ambayo inatumiwa na wanafunzi wa kata zote mbili (Bulongwa na Luwumbu).

Mh. Luvanda amesema “tulikubaliana na wenzetu wa Luwumbu kwamba Bulongwa tunampango wa kujenga shule yetu na hatuwezi kushiriki Luwumbu ambapo wanapaswa kuongeza nguvu kwa 20% tu”

Kitulo Fm imezungumza na Mwenyekiti wa Kijiji cha Bulongwa Gabriel Sanga ambaye amesema wananchi wa kijiji cha Bulongwa hawana taarifa za ujenzi huo, huku Mratibu Elimu Kata ya Bulongwa Mwl. Fedson Muholi akiongeza kuwa wakati akishiriki kwenye vikao vya KAMAKA hakuna taarifa yeyote ya wananchi kukataa kushiriki ujenzi wa bweni shuleni usililo”

Mtendaji Kata ya Luwumbu Bi. Evelina Sanga amesema makubaliano ya kikao cha mwezi Disemba 2021 ilikuwa  ni kuhakikisha viongozi wa Kata ya Bulongwa wanaenda kuwashirikisha wananchi wao kuhusu ujenzi wa bweni hilo ili kuwa na nguvu za pamoja

Amesema mpaka sasa hawajapata majibu yoyote kutoka kwa viongozi wa Kata ya Bulongwa kuhusu ushirikishwaji huo na ujenzi wa bweni hilo ulishaanza kwa nguvu za wananchi wa Kata ya Luwumbu pekee wanaochangia asilimia 20 huku Serikali kupitia TASAF ikichangia asilimia 80

Diwani wa Kata ya Luwumbu Mh. Felix Kyando amesema anashangaa kuona wananchi wa Kata ya Bulongwa pamoja na Diwani wao hawataki kushiriki ujenzi wa bweni ambapo watoto wengi wanaosoma shuleni hapo wanatoka Kata ya Bulongwa, huku akiomuomba Diwani wa Bulongwa kutoa ushirikiano kwenye ujenzi huo.

SOMA HII;FAHAMU MAMBO YANAYO CHANGIA MWANAMKE KUKOSA HISIA ZA MAPENZI

Wiki iliyopita Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh. Juma Sweda alimuagiza Afisa Tarafa, Tarafa ya Bulongwa kuitisha kikao cha viongozi Kata ya Bulongwa na Luwumbu kujadili na kufikia mwafaka wa kushirikiana kwenye ujenzi huo

Kata ya Bulongwa mpaka sasa haina shule ya Sekondari na wanafunzi wanaotoka Kata hiyo yenye vijiji vitano wanasoma Kata ya Luwumbu

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top