DPP AWAFUTIA MASHITAKA WAFANYAKAZI 6 TMDA

0

 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaachia huru wafanyakazi sita wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi dhidi yao.

DPP awafutia mashitaka wafanyakazi 6 TMDA

Walioachiwa huru ni Charys Ugullum, Raymond Wigenge, Ezekiel Mubito, Adelard Mtenga na Abdallah Juma, ambao walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh bilioni 58.3 kwa kujilipa posho.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Hassan Dunia, Mei 17, 2022, amedai  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ritha Tarimo kuwa DPP amewasilisha maombi ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Tarimo alikubali ombi la upande wa mashitaka kwa kufuta kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 5 ya 2018  na kuwaachia huru washitakiwa.

Ilidaiwa kuwa kati ya Mei na Desemba 2016 katika Ofisi za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA wakati huo) waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh 58,390,000 fedha ambazo ni posho za wafanyakazi waliokuwa wamesaini malipo yao, jambo lililosababisha kujilipa mara mbili.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top