
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 4 Mei 2022. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-
(a) Bei za rejareja za petroli ni Shilingi 3,148 kwa lita kwa Dar es Salaam, Shilingi 3,161 kwa lita kwa Tanga na Shilingi 3,177 kwa lita kwa Mtwara;
(b) Bei za rejareja za dizeli ni Shilingi 3,258 kwa lita kwa Dar es Salaam, Shilingi 3,264 kwa lita kwa Tanga na Shilingi 3,309 kwa lita kwa Mtwara;
(d) Mabadiliko ya bei yanatokana na ongezeko la bei za mafuta katika soko la dunia zinazochangia takribani asilimia 93 ya ongezeko la bei hizo na gharama za uagizaji (premium) ambazo zinachangia takribani asilimia 4. Vilevile, bei za mafuta hapa nchini zina uwiano na bei za bidhaa hizo katika nchi jirani.
