FAHAMU SABABU ZA MWANAMKE KUBLID DAMU NYINGI NA KWA MDA MREFU....

0

Mwanamke akianza hedhi, kwa kawaidia humaliza katika siku tatu hadi tano. Hedhi inayochukua zaidi ya siku saba tunasema ni hedhi ndefu. Kitaalamu, hedhi inayozidi siku saba huitwa menorrhagia.

 Asilimia tano ya wanawake wana menorrhagia. Katika ukurasa huu, tutalijadili tatizo la kutoka damu siku nyingi au kwa lugha nyingine, tatizo la kuwa na period ndefu.

Hedhi ndefu ni dalili ya tatizo la kiafya, kama matatizo ya:

. mabadiliko ya mpangilio wa homoni
. matatizo ya nyumba ya kizazi
. Saratani

Hedhi ndefu huweza kusababisha kukosa raha wakati wa hedhi au hata kuvuruga shughuli za kawaida. Hedhi ndefu yaweza pia kuvuruga usingizi wako. Hedhi ndefu huweza kusababisha upungufu wa madini ya chuma, na hasa hedhi hizo zikiwa nzito.

Tatizo hili limekuwa likiwasumbua wanawake wengi sana kwa hivi sasa na huku wengine mbali na kublid mda mrefu pia mzunguko mzima wa hedhi umekuwa wa kutokueleweka kabsa. Mfano; mara apitishe miezi miwili bila kuona siku zake, mara aone mara mbili ndani ya mwezi Mmoja N.k

Tunasema mwanamke ameblid kwa Mda Mrefu hasa pale period inapotoka kwa zaidi ya Siku Saba Mfululizo. Hilo ni tatizo.

Nini Kinasababisha Kuwa Na Period Ndefu?

Hedhi ndefu ni matokeo ya hali nyingi zinazotokana na afya yako, umri wako na staili yako ya maisha. Baadhi zikiwa:

Mabadiliko Ya Homoni Na Utolewaji Wa Yai

Kama homoni zako haziko kwenye viwango vizuri au kama mwili wako hauachii yai katika mzunguko wako wa hedhi, ngozi laini (uterine lining) inayotanda juu ya nyumba ya uzazi huwa nene sana. Mwili wako baadaye unapoondoa utando huu, unaweza ukaona unapata siku nyingi zaidi za hedhi.

Madawa

Unaweza ukaingia period kwa siku nyingi kwa sababu ya dawa unazozitumia. Dawa hizi ni pamoja na:

. dawa za kuzuia mimba
. aspirin na blood thinners
. Anti-inflammatories.

Ujauzito

Kutoka damu kwa muda mrefu kunaweza pia kuwa ni ishara ya matatizo ya mimba, kama mimba iliyotungwa nje ya kizazi (ectopic pregancy) au kuharibika kwa mimba (miscarriage).

Unaweza kuwa na hedhi ndefu kwa sababu ya tatizo la placenta previa, placenta ya mtoto kuziba kwa kiasi fulani au kuziba kabisa cervix. Placenta previa inaweza kusababisha kutoka damu kwa wingi wakati wa ujauzito au wakati wakati wa kuzaa. Ukiwa na placenta previa unaweza kutoka damu mfululizo kipindi chote cha ujauzito.

Uvimbe (fibroids) au Polyps

Uvimbe kwenye kizazi (fibroid na polyps) huweza kusababisha hedhi ndefu, na wakati mwingine kutoka damu kwa wingi.

Fibroids ni kujenga kwa tishu za misuli kwenye kuta za nyumba ya uzazi (uterus).

Polyps ni matokeo ya kujenga kusiko kwa kawaida kwa tishu ndani ya nyumba ya uzazi na kusababisha uvimbe mdogo.

Kwa kawaida, fibroids na polyps si uvimbe wa saratani.

Adenomyosis

Adenomyosis ni aina nnyingine ya kujijenga kwa tishu. Hali hii hutokea pale endemetrium, au ngozi laini ya juu ya nyumba ya uzazi, inapoungana na misuli ya uterus. Hii huweza kusababisha kupata hedhi ya muda mrefu.

Tezi ya Thyroid

Unaweza kupata hedhi kwa muda mrefu kama tezi yako ya thyroid inatenda kazi chini ya kiwango chake. Hali hii huitwa hypothyroidism.

Kutokwa damu

Unaweza kuwa na hali ambayo imeathiri uwezo wa mwili wako kuifanya damu yako igande, na kukusababishia hedhi ndefu. Mbili katika hali hizi ni hemophilia na von Willebrand’s disease.

Unene

Unene uliozidi unaweza kukusababisha kuingia period kwa muda mrefu. Hapa ni kwa sababu tishu za mafuta zinaweza kusababisha mwili kutengeneza estrogen nyingi zaidi. Estrogen hii ya ziada inaweza kukuletea mabadiliko ya hedhi yako.

Ugonjwa wa PID

Pelvic inflammatory disease (PID) hutokea pale bakteria wanaposhambulia viungo vyako vya uzazi. Pamoja na kubadlisha mzunguko wako wa hedhi, PID inaweza kusababisha kutoka uchafu usio wa kawaida pamoja na dalili nyingine.

Saratani

Kutoka damu kwa muda mrefu wakati wa hedhi inaweza kuwa ni ishara ya saratani katika nyumba ya uzazi au shingo ya kizazi. Kwa baadhi ya wanawake, hii inaweza kuwa ndiyo dalili ya kwanza ya saratani hizi.

 Jee, Unaweza Kufupisha Siku Zako Za Hedhi?

 Ni kitu cha kawaida kutokea kuwa utasafiri nje ya nyumbani kwako, ukataka kwenda beach, ukawa na shughuli fulani muhimu, na tarehe zikagongana na siku zako za hedhi. Kuliko kuahirisha plani zako, unaweza kuzipunguza siku za hedhi katika mzunguko wako.

Kuna mbinu unazoweza kuzijaribu ili hedhi yako iishe mapema zaidi. Baadhi ya mbinu hizi unaweza kuzifanya kila mwezi bila madhara, lakini nyingine zinahitaji ushauri wa daktari.

1. Tumia vidonge vya uzazi wa mpango (hormonal birth control pills)

Vidonge vya uzazi wa mpango (Oral birth control pills) na sindano (birth control injections) vinaweza kutumika kuidhibiti hedhi yako. Vidonge vinaweza pia kupunguza maumivu ya tumbo na kupunguza siku za hedhi kila mwezi. Ukianza kutumia vidonge hivi sasa, itakuchukua miezi kadhaa kabla hedhi yako haijapungua siku zake.

hedhi ndefu vidonge

Yafaa kupata ushauri wa daktari kuhusu vidonge vitakavyokufaa.

2. Fanya tendo la ndoa

Kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa, kunaweza kupunguza maumivu ya tumbo na utokwaji wa damu. Hii ni kwa sababu kufika kileleni kunasababisha kukaza kwa misuli ya nyumba ya uzazi, tendo ambalo litasaidia kuiondoa damu kwenye nyumba ya uzazi.

Kukaza huku kwa misuli kunasaidia nyumba ya uzazi kumwaga damu haraka.

3. Fanya mazoezi mara kwa mara

Kuwa na ratiba ya kufanya mazoezi ya kuhema haraka (cardiovascular exercise routine) hakusaidii kuboresha afya tuu, lakini pia husaidia kupunguza uzito wa hedhi. Kunaweza pia kusaidia kupunguza idadi ya siku za hedhi unazopata. Mazoezi pia hupunguza maji mwilini, na kuzuia tumbo kujaa na maumivu ya hedhi.

hedhi ndefu mazoezi

Yafaa kujua mazoezi mazuri ya kuyafanya. Mazoezi ya kuzidi kipimo yanaweza kukufanya ukonde sana hadi chini ya kiwango kinachofaa, kitu ambacho kinaweza kuvuruga afya yako ya homoni na kukufanya usimame hedhi.

4. Linda uzito wako wa mwili

Mabadiliko katika uzito wako huathiri hedhi zako na kuzifanya kuwa zisizoeleweka. Kwa kawaida, wanawake wenye uzito mkubwa wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata hedhi nzito. Wanawake wengine wanaweza kupata hedhi nzito, zenye maumivu kwa wiki kadhaa. Hii hutokana na kuzalishwa kwa estrogen kwa wingi kutoka seli za mafuta, ambako kunaweza kuleta hedhi ndefu na nzito.

5. Pata virutubishi

Baadhi ya virutubishi, kama vitamini B, ni muhimu kwa afya yako ya jumla. Baadhi vinaweza kukulegezea hedhi zako na kukuondolea maumivu ya wakati wa hedhi.

Vitamini B6 ni moja ya virutubishi vyenye mchango kwenye hedhi yako. Vitamini hii hupatikana ndani ya baadhi ya chakula kama mayai, samaki, na kuku. Vitamini B6 imebainika kuongeza homoni ya progesterone wakati ikipunguza estrogen ndani ya mwili. Hii inaweza kuisaidia tezi ya pituitary kuweka vizuri homoni za hedhi.

Utafiti mwingine ulionyesha kuwa zinc inasaidia kupunguza maumivu ya hedhi.

Magnesium ni madini mengine yenye uwezo wa kuondoa hedhi ndefu, zenye maumivu. Mchanganyiko wa magnesium na B6 umeonyesha kutoa msaada wa kupunguza maumivu ya hedhi.

6. Jaribu mimea ifuatayo

Baadhi ya mimea huweza kupunguza hedhi ndefu na zenye maumivu. Mimea ambayo imeonyesha matumaini ni pamoja na:

. fennel (shamari-kiungo jamii ya karoti), mmea wenye tabia ya kutuliza maumivu na kuzuia uvimbe unaoweza kupunguza maumivu ya hedhi na urefu wa hedhi
. Tangawizi, inayoweza kupunguza hedhi nzito
. raspberry leaf, yenye tabia ya kulegeza misuli itakayopunguza kukaza kwa misuli ya nyumba ya uzazi

7. Kunywa maji mengi.

Linapokuja swala la kupunguza makali ya hedhi, kunywa maji mengi ndiyo msingi.

hedhi nzito kunywa maji

Kama unywaji wako wa maji ni chini ya glasi 8 kwa siku, jaribu kuongeza kiwango ukiwa ndani ya hedhi – hii itakusaidia kupata maumivu kidogo zaidi na kupunguza maumivu ya kichwa. Inaweza kukusaidia kuongeza kasi ya mzunguko wako wa hedhi. Unywaji wa maji huzuia damu isiwe nzito.

Tafadhali tunaomba SHARE post hii kupitia mitandao yako ya akijamii utabarikiwa kuwasaidia wengine,kwa maswali na ushauri kuhusu masuala ya afya wasiliana na DrAman Ezekiel kwa number 0765 366 133.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top