FAHAMU UGONJWA WA PELVIC INFAMMATORY (PID) NA JINSI YA KUJIKINGA

0

 Mara nyingi , imekua ni vugumu watu kutofautisha PID na magonjwa mengine ya njia ya uzazi.

Athari ya kutokujua tatizo ni vigumu pia kupata tiba sahihi ya tatizo, hali ambayo inaweza sababisha viungo vingine vya uzazi kuzidi kuathirika zaidi.


Lakini kwanza hebu tujifunze kwa kina nini hasa ugonjwa wa PID.

Neno PID ni kifupi cha neno Pelvic Inflammatory Disease.

Haya ni maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke, viungo hivyo ni mirija ya uzazi (Fallopian tubes), via vya mayai (ovaries), mlango wa njia ya uzazi (cervics) na kuta za mfumo wa uzazi (uterus).

Maambukizi haya husababishwa na aina mbalimbali za bacteria sawa na wale wanaosababisha magonjwa ya kisonono na kaswende.

Utofauti wake ni kwamba, maambukizi haya ya magonjwa ya ngono yanapozidi kua sugu huhamia katika viungo vya ndani kabisa vya uzazi (pelvis) na hatimae huhamia katika mzunguko wa damu.

Ugonjwa huu ni hatari kwa afya, hivyo ni bora kujitibu mapema kabla tatizo halijawa kubwa.

Athari za ugonjwa huu usipodhibitiwa mapema ni hizi;

↔Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy).

Hii ni kasoro inayojitokeza pindi PID inapokua haijatibiwa kwa muda mrefu, bacteria hushambulia kutaza za mrija wa uzazi (fallopian tubes) na kusababisha yai lilorubishwa kushindwa kupita kuelekea katika mji wa mimba (uterus).


Badala yake , yai liloshindwa kupita hujipandikiza katika mrija wa uzazi (fallopian) , hali ambayo ni hatari sana kwa usalama wa afya.

↔Kushindwa kushika mimba (infertilty) au kuharibika kwa mimba kila mara.

Hii inatokana na viungo vya uzazi kuathirika pakubwa.

↔Maumivu makali ya tumbo na kutokwa damu nyingi , hali ambayo inaweza pelekea upungufu wa damu na kupoteza maisha.

↔Saratani ya mlango wa uzazi (cervix cancer).

PID isipotibika mapema, maambukizi yake husababisha uchafu (usaa) kujikusanya hasa katika mirija ya uzazi (fallopian tubes) na via ya mayai (ovaries) vivile katika kuta za uzazi (uterus) na kusababisha saratani ya uzazi.

Hali ambayo inaweza sababisha kufanyiwa operation na kutolewa kizazi au kupoteza maisha endapo haitatibika mapema.

Je, PID inaenezwa vipi?

Maambukizi ya PID huenezwa kwa njia ya tendo la ndoa.

Endapo kama utashiriki tendo la ndoa na mwanaume bila kinga na akawa yuko na partner mwingine ambae ana ugonjwa wa PID anaweza kukuambukiza na wewe pia.

Pia matumizi ya vifaa vya kuingiza katika njia ya uzazi (intrauterine devices), hii inajumuisha pia njia ya uzazi (kitanzi) endapo kama usafi hautazingatiwa , inaweza sababisha maambukizi.

Lakini je, utajuaje kama una ugonjwa wa PID?


Ukijihisi dalili zifuatazo, anza mapema kabisa kujitibu bila kukawia.

Je, unahisi dalili hizi?

  1. Je, Maumivu makali wakati mwingine unatokwa na damu baada ya kushiriki tendo la ndoa?
  2. Je, Unatokwa na uchafu mweupe unaoelekea kua na njano na harufu kali kama maji ya samaki?
  3. Je, unatokwa na damu nyingi wakati wa hedhi au baada ya tendo la ndoa?
  4. Je, unapata homa kali inayoambatana na maumivu ya tumbo chini ya kitovu?
  5. Je, mimba zako zinatunga nje ya mfuko wa uzazi na kuharibika mara kwa mara?
  6. Je, ulifanya uchunguzi na ukapewa dawa za magonjwa ya zinaa hospitalini ila hali yako bado inakutesa?
  7. Umeshachoma sindano , umemeza vidonge ila hali yako kiafya haiko sawa kabisa, bado tatizo linakutesa?

Ikiwa majibu yako ni ndiyo, basi ni wazi kua uko na tatizo la PID!

watu wengi niliowatibu PID walishapitia changamoto nyingi sana ikiwa ni pamoja na kutumia dawa mbalimbali bila mafanikio.

Ila sasa, kwakua umeweza kuwasiliana na mimi na makala hii umeielewa kwa kina, huu ndio mwanzo wa kukomesha na kulitokomeza kabisa tatizo lako.

Ushirikiano baina yangu na wewe tunaenda kulitokomeza tatizo hili ndani ya siku 14 tu, kama wengine walivyoshirkiana na mimi wakafanikiwa.

Lakini je, mtu atajikinga vipi na PID?

Ili upate kujikinga dhidi ya PID unapaswa kuzingatia taratibu zifuatazo;

  1. Usafi.

Hakikisha nguo za ndani (chupi) zinakua safi , na kila ukiingia uwani basi nawa kwa maji ya kutosha.

Zingatia utaratibu wa kujisafisha njia ya mkojo kwanza ndipo umalizie na njia ya hajakubwa, hii itakusaidia usiwahamishe bacteria kutoka njia ya hajakubwa na kuwaleta njia ya uzazi/mkojo.

  1. Epuka ngono nzembe.

Epuka kua na mahusiano na wanaume wengi, pia tumia kinga (condom) kama utashiri tendo na mwanaume usiemuamini na hamjapima afya.

  1. Epuka vipodozi vyenye kemikali.

Sabuni, mafuta au marashi yenye kemikali, huua bacteria rafiki wanaolinda ngozi na viungo vya mwili (normalflora), hivyo viepuke kujisafisha, kuogea au kujipakaa na kujipuliza katika sehemu za chini (viungo vya uzazi).

  1. Jitibu magonjwa letekezi.

PID huletekezwa na magonjwa mengine ya zinaa (kisonono, kaswende na UTI) pindi magonjwa haya yasipotibika mapema , huingia ndani zaidi ya mfumo wa uzazi/mkojo na kuanza kushambulia.

Sasa ili kuepuka tatizo hili inakubidi uwahi kufanya vipimo na kujitibu kabla tatizo halijawa sugu na kubadilika kua PID.

  1. Kula vyakula vyenye kuimarisha kingamwili.

Hakikisha unakula matunda yenye vitamin C kwa wingi, mbogamboga na maji ya kutosha ili, kuimarisha kinga za mwili (body immunity) itakokukinga dhidi ya maradhi letekezi ya PID.

Endapo tatizo lako litakua sugu sana na umejaribu kufanya tiba mbalimbali bila mafanikio, nakukaribisha katika program yangu ya tiba ndani ya siku 15.

Program hii inahusisha lishe, usafi na tiba mimea. Kuzingatia taratibu zote basi kuanzia leo ndio mwanzo wa furaha yako na utaondokana na tatizo hili.

Somo hili limeletwa kwako na 

Lomalinda Sanitarium Clinic.


Dr.Amani Ezekiel Buchafwe

Call/sms 0765 366 133/ 0715 943 838

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top