Halima Mdee: Kilichotokea kufutwa uanachama ni uhuni Hata Mbowe anajua

0

 Mbunge Halima Mdee kwa niaba ya wenzake 18 ameelezea kutokubaliana na uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wa kutupilia mbali rufaa zao za kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya Chama hicho akisema kilichofanyika ni uhuni.

"Nakwepa kuzungumza maneno makali kwasababu naheshimu Viongozi wangu lakini sikujua CHADEMA umeanza kufanyika uhuni kwa kiwango hicho, Mimi ni CHADEMA naendelea kuwa CHADEMA lakini kilichofanyika pale uhuni wa kiwango cha hatari , nitaongea siku nyingine lakini kilichofanyika pale hata Mbowe anajua ni uhuni"

Mdee ambaye amepata kuwa mbunge wa Jimbo la Kawe na Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema, Bawacha, ni miongoni mwa makada walifukuzwa baada ya Bazara Kuu kubariki uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kuwafukuza ndani ya chama kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge kinyume cha matakwa ya chama hicho.

    Matokeo ya jumla baada kupigwa kura

  1. Idadi ya wajumbe 423

  2. Waliokubalina na maamuzi ya Kamati ya kuwafukuza Uanachama ni 413 sawa 97.6%
  3. Wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati kuu ni 5 sawa na 1.2%
  4. Wasiofungamana na upande wowote ni 5 sawa na 1.2%

JE! NINI KINAFUATA BAADA YA KUVULIWA UANACHAMA?

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amesema kwa sasa hakuna nafasi nyingine kwa waliokuwa makada 19 wa chama hicho ya kukata rufaa. 

Pia, amesema hatua inayofuata ni Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kuandika barua ya kumtaarifu Spika wa Bunge kuhusu uamuzi uliofanywa na baraza kuu kwa hatua zaidi ikiwemo ya kutangazwa kuvuliwa ubunge.

Baada ya Mbunge Halima Mdee kwa niaba ya wenzake 18 kutokubalina na uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wa kutupilia mbali rufaa zao za kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya Chama hicho akisema kilichofanyika ni uhuni, Mbowe amemjibu na kuwaambia wao ndio waache uhuni.

“Nimesikitika hatujafurahia hali hiyo ila imebidi, maamuzi ya kuwafukuza yalifanyika tangu mwaka juzi kwenye kikao cha Kamati Kuu, kura zimepigwa mbele yao waache mambo ya kihuni”


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top