HII NDIO PETE YAKUJIKINGA NA HIV! IFAHAMU.

0

Wakati wataalamu wakiendelea na utafiti wa dawa ya kutibu ukimwi, imegundilika mbinu mpya ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa wanawake kwa kutumia pete maalumu iitwayo ‘Dapivirine Vaginal Ring’. 

Pete hiyo ambayo inapewa nafasi kubwa ya kushusha maambukizi kwa kundi hilo, ina madini ya silikoni inayovaliwa ukeni na hudumu kwa siku 28 na hutoa dawa kinga ya ‘dapivirine’ inayoua virusi vya ukimwi ukeni.

 Imeelezwa kuwa ni rahisi kuivaa, inakinga virusi kwa asilimia kubwa na hata mwenza hawezi kubaini iwapo mwanamke ameivaa. 

Ujio wa pete hiyo umetokana na utafiti wa muda mrefu uliolenga kutafuta njia ya kuwalinda wanawake dhidi ya maambukizi ya VVU wakati wa kujamiiana bila kutegemea wanaume kuvaa mipira (kondomu). 

Kinga hiyo imekuja baada ya utafiti wa miaka zaidi ya 10 kufanyika nchini Marekani na Afrika na mwaka 2020 Shirika la Afya Duniani (WHO) liliruhusu pete hizo kutumika kama njia ya kinga na mpaka sasa nchi nne zimeanza kutumia ikiwemo Afrika Kusini, Uganda, Zimbabwe na Malawi. 

Kwa upande wake, Serikali imekiri kuifuatilia pete hiyo na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifelo Sichwale alipoulizwa alisema Wizara ya Afya ina taarifa na uwepo wa kinga hiyo mpya. 

“Taarifa pia zimepokelewa kupitia asasi zisizo za kiserikali (CSOs) pamoja na umoja wa wanawake wanaoishi na maambukizi ya VVU wakihimiza upatikanaji na matumizi ya dawa yaanze. 

Wataalamu wizarani kupitia NACP (Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi) watashirikiana na Taasisi ya utafiti na TMDA (Mamkala ya Dawa na Vifaa Tiba) kuendelea na mjadala kuangalia ubora na usalama wa dawa hiyo kabla ya kuanza kutumika nchini na kama ina faida zaidi ukilinganisha na kinga za aina nyingine zinazotumika,” alisema Dk Sichwale 

Credit:MCL Digital.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top