HIZI NDIO SABABU 7 KWANINI BIASHARA ZINAKUFA MAPEMA.

0

Utafiti wa SBA umetaja zifuatazo ni sababu kubwa zinazosababisha biashara nyingi ndogo zife mapema:

Kuanzisha biashara kwa sababu zisizo sahihi; Kwa mfano, mtu anataka kuanzisha biashara kwasababu tu ataki kuajiriwa hivyo anaamini akiingia kwenye biashara atakuwa FREE na atakuwa na muda wa kutosha wakutumia na familia yake wakati kiuhalisia biashara inahitaji muda sana kwenye kusimamia hivyo unaona sababu ya mtu kama huyu kuingia kwenye biashara ni tofauti kabisa na uhalisia wa biashara.

Sababu sahihi za kuingia kwenye biashara ni kama, mtu umeona kuna tatizo ambalo unaweza kulitatua kupitia biashara au mtu umeona kuna uhitaji mkubwa wa kitu fulani na wewe unaweza kufanikiwa kutatua uhitaji uo kupitia biashara.

Usimamizi mbaya; biashara ndogo zinakufa mapema kwasababu ya usimamizi mbaya.Biashara inaanza bila kuwa na msimamizi wa mambo mbalimbali kama masuala ya kifedha na mambo mengine ya biashara matokeo yake biashara inakufa.

Shida nyingine ni pale mfanyabiashara mdogo anakuwa na majukumu zaidi ya 5 ambayo hayuko na ufanisi nayo. 

Unakuta mfanyabiashara anafanya biashara na hata hatunzi taarifa zake za mauzo na matumizi, kwa nini io biashara isife?

Mtaji mdogo; mtaji mdogo ni sababu inayochangia biashara nyingi kufa mapema kwasababu ikitokea tu kuna hasara kubwa kwenye biashara basi kuna asilimia kubwa za biashara iyo kufa kwasababu haina mtaji ambao unaweza kuifanya ikajiendesha wakati wa hasara.

Kutokuwa sahihi na eneo la biashara; Kuna wafanyabiashara wanabidhaa sahihi lakini sehemu walipo ni changamoto.Mfano ni mtu kuwa na bidhaa za ufahari kisha sehemu ya biashara yake ni eneo la watu wa hali ya chini kifedha.

Kukosa mpango wa biashara; biashara nyingi ndogo hazina mpango wa biashara na hazifanyi utafiti kuhusu biashara zao.Biashara ndogo hazina mpango wa wapi zinataka kuwa ndani ya miaka 5 ijayo na hazina mikakati ya kuendeleza biashara zao.

Kujitanua mapema; biashara ndogo uwa zinataka kujitanua mapema kwa kufungua matawi ya biashara zake zaidi ya sehemu 1 kabla hata ya kuwa imara na biashara au sehemu ya mwanzo.

Kushindwa kwenda sawa na mabadiliko ya teknolojia kwenye biashara.share ujumbe huu kupitia kitufe cha WhatsApp hapo chini.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top