KAYA MASIKINI KUSAIDIWA VIBAO VYA ANWANI ZA MAKAZI

0

Ili kuhamasisha na kufikia malengo ya serikali pamoja na halmashauri katika uwekaji wa vibao kwenye nyumba kupitia zoezi la anwani ya makazi,diwani wa kata ya Uwemba halmashauri ya mji wa Njombe bwana Jactan Mtewele ameahidi kununua na kuweka vibao katika kaya masikini zote zilizopo katika kijiji cha Kilenzi.

Mtewele amebainisha hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika eneo la mradi wa maji kwa ajili ya Kilenzi uliopo katika kijiji cha Njomlole

“Nitawasaidia kaya masikini kuweka vibao na hii yote nataka tuhamasishe zoezi la uwekaji wa vibao vya anwani za makazi”Alisema Jactan Mtewele diwani wa kata ya Uwemba

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top