Afisa Mtendaji Kata ya Kingachi, Issa Maringo katika kikao cha Kamati ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukatili wa Kijinsia ametaja kuyumba kiuchumi na kushindwa kuwajibika katika malezi ya familia kwa baadhi ya Wanaume ni moja ya sababu za kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya kikatili na wake zao.
![]() |
Picha kutoka maktaba! |
Amesema kumekuwepo na vikundi vingi vya kuwezesha Wanawake kiuchumi hivyo kumiliki uchumi na kuwaacha Wanaume nyumbani. Hii imesababisha baadhi ya Wanaume kuwa walevi wa kupindukia na kuambulia vipigo kutoka kwa wake zao
Aidha, Erenia Kimaro (Mjumbe wa Kamati hiyo) alisema ipo haja kwa Serikali na Mashirika yanayotetea Wanawake, kuwatazama Wanaume na kuona namna ya kuwawezesha kiuchumi ili kuondokana na manyanyaso