Jamii imetakiwa kutumia taulo za kike zilizo salama ili kulinda afya zao na kuchukulia suala la hedhi salama ni jambo la kawaida ambapo kila mmoja anapaswa kulizungumzia na kumsaidia muhitaji kujisitili wakaati wa hedhi hasa wanafunzi.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja huduma kwa wateja kutoka LAVY PADS Products Nasra Bernard Msekwa wakati akizungumza na Kituo cha Redio Green fm kilichopo wilayani Makete Mkoani Njombe ambapo amesema mwananchi au mfanyabiashara kila anaponunua anakuwa sehemu ya kumsaidia mtoto wa kike kutimiza ndoto zake za kielimu.
Amesema kuwa asilimia 10% ya mauzo imekuwa ikipelekwa kwa ajili ya wanafunzi wasio na uwezo wa kumudu gharama za kununua taulo za kike wawapo shuleni hivyo Lavy Pads wamekuwa wakipatia bure kutokana na wateja wanaotumiaa bidhaa hiyo.
Bi Nasraa Msekwa ameitakaa jamii kutumiaa bidhaa hiyo ili kuwa sehemu ya kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji.
TAZAMA VIDEO HII AKITOA USHUHUDA JINSI LAVY PADS ZILIVYOCHANGIA UFAULU WA WANAFUNZI.