MACHINGA WAANDAMANA NA KUFUNGA BARABARA KWA KUTUMIA BIDHAA ZAO

0

Wafanyabiashara wadogo (Machinga) waliondolewa maeneo yasiyo rasmi na kupangwa katika  Soko la Msufini Mjini Geita Mapema leo wameandamana na kufunga barabara kuu katikati ya mji wakidai Serikali imeshindwa kuwarudisha kwenye soko lao wafanyabiashara ambao wamehama kutoka kwenye soko hilo na kurudi  kwenye maeneo ya zamani yasiyo rasmi.

Machinga hao wamefunga barabara Kwa kutumia bidhaa zao kama nyanya ,pilipili,viazi kwa kuzipanda katikati ya barabara na kuzuia kusababisha huduma kusimama Kwa muda kabla ya kuondolewa na Jeshi la Polisi bila usumbufu.

Wafanyabiashara hao wanasema wenzao wamerudi kwenye maeneo ya zamani yasiyo rasmi hivyo wateja wamelazimika kuwafuata huko huko mtaani na kusababisha wao kupata hasara kwasababu wanakosa wateja.

Wamesema kuwa bidhaa zao zinakosa wateja na kuozea sokoni na kusababisha wapate hasara, hivyo wameandamana ili Serikali iweze kuwasikiliza na kuwaondoa waliorudi maeneo yasiyo rasmi ili warudi sokoni ili wateja waweze kwenda kununua bidhaa sokoni.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Constantine Morandi amesema amepata taarifa za maandamano hayo na kwamba ana taarifa za machinga wachache kurudi taratibu maeneo ya barabarani yasiyo rasmi.

Amesema anawasihi wamachinga waliorudi maeneo yasiyo rasmi kuondoka na kurudi kwenye masoko rasmi ya Nyankumbu,Katundu na Msufini.

Ameeleza kuwa amekutana na viongozi wa Machinga na wamekubaliana kuwashauri wenzao waliorudi maeneo yasiyo rasmi kuondoka kurudi kwenye masoko rasmi ambayo yameandaliwa kwani miundombinu yote ilisha kamilika.


Mkurugenzi wa Mji wa Geita Zahara Michuzi amesema Halmashauri imewekeza zaidi ya Bilioni Moja kwenye soko la Katundu na limekamilika,lakini soko la Msufini miundombinu imejengwa hivyo amewataka kuondoka barabarani na kurudi kwenye masoko hayo .

Mauld Said Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Geita amesema kuwa wamewasilisha malalamiko yao kwa viongozi wa Serikali lakini wamekuwa hawapati majibu ndiyo maana wameamua kuangamana.

Credit:Mwangaza tv.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top