Wilberforce Murunga (52) ameshinda kesi dhidi ya waliokuwa Shemeji zake ya kutaka arudishiwe mahari ya pesa na mali alizotoa kwa ajili ya kumuoa Irine Mitekho Khaoya katika ndoa ambayo ilidumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu
Murunga alilipa mahari ya Ksh. 50,000 (Tsh. 988,908), Mifugo na Viatu (gumboots na kofia). Alitalikiana na mkewe ambaye inadaiwa hakuwa mwaminifu kwenye ndoa, ndipo akafungua kesi ya kutaka shemeji zake wamrudishie mahari
Mahakama ya Kitale ilimpa ushindi huo na kumtaka Murunga apewe alichokitaka, lakini baada ya mazungumzo wakakubaliana atapewa ng’ombe mmoja na Ksh. 30,000 (Tsh. 593,345) kama fidia ya mahari aliyoitoa Aprili 27, 2019.
Hata hivyo, mwaka mmoja na nusu baadaye, ndoa yao ilianza kusambaratika baada ya mke kudaiwa kuanza kuwa na mipango ya kando.
Hii ilikuwa baada ya Murunga kusafiri hadi Marekani kwa masomo zaidi lakini akasema alilazimika kukatiza shughuli hiyo baada ya mkew kumwarifu arejee nyumbani ili wapate watoto.
“Mke wangu ndiyo sababu ya mimi kurudi kutoka Marekani baada ya miaka miwili, nilikuwa namtumia pesa, lakini aliponiambia nirudi nyumbani tuzae sikuwa na jinsi zaidi ya kurudi nyumbani,” alisema Murunga.
Chanzo;tukoswahili